Wanafunzi Chuo Kikuu wabakwa, walawitiwa

Wanafunzi Chuo Kikuu wabakwa, walawitiwa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
[h=2]Thursday, May 31, 2012[/h][h=3][/h]

05_12_0qj8nn.jpg

Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma

WANACHUO wa Chuo Kikuu cha St John mjini Dodoma, leo wamegoma kuingia
madarasani hadi wawasilishe malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi wa
Mkoa, Zelothe Stephen kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa
nondo, kuibiwa kadi za benki, kompyuta za mkononi, kulawitiwa na
kubakwa.

Hali hiyo ilisababisha wanafunzi kukusanyika huku wakiwa wamebeba
mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yakisomeka, ‘Tunaomba ulinzi ili
kubaka na kulawitiwa kukomeshwe’, ‘Ulinzi ni haki yetu ya msingi polisi
Mko wapi? Tumechoka kuwa wajinga katika jamii yetu na Ulinzi Shirikishi
stop crime.’

Baadhi ya wanafunzi hao walilaani vitendo vya wenzao kubakwa na
kulawitiwa na kudai kuwa katika siku za hivi karibuni, mwanafunzi wa
kiume ambaye anasoma mwaka mwaka wa pili aliibiwa na kisha kulawitiwa
hali iliyolazimu alazwe hospitali.

“Kesi kadhaa zimepelekwa polisi lakini hakuna chochote kinachofanyika,” alisikika mwanachuo moja akizungumza kwa jazba.

Walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu
kutokana na kuibiwa vifaa muhimu zikiwemo kompyuta za mkononi hali
ambayo hulazimika kuishi kwa hofu.

“Juzi wenzetu wamevamiwa usiku na kuporwa simu tano na laptop tatu
sasa tunaona maisha yanakuwa magumu sana kwetu kwani usalama wetu sasa
ni mdogo,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Walisema hali ni mbaya zaidi kwa wanafunzi ambao wanaishi nje ya
chuo kwani hata kujisomea nyakati za jioni kumekuwa kwa mashaka
kutokana na kuogopa kuvamiwa na vibaka.
Walisema baadhi ya wenzao wanaanza mitihani Juni, hali ambayo
inawatia hofu kama wimbi hilo la kuvamiwa na vibaka linaweza hata
kupunguza ufaulu mioungoni mwao.

Pia walitaja sababu kadhaa ambazo zinadhaniwa kuwa zinasababisha
matukio hayo ni chuo hicho kukosa uzio na hivyo kufanya mwingiliano wa
watu na wanachuo kuingia chuoni bila kuwa na utaratibu.

Walisema kundi lisilojulikana limekuwa na kawaida ya kuvamia sehemu
ambazo wanachuo wanakaa na baada ya kuiba vitu mbalimbali humalizia kwa
kubaka wasichana au kwa kulawiti kama ni mvulana.

Hata hivyo, juhudi za wanafunzi wao kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Dodoma hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa alikuwa na majukumu
mengine ya kikazi, na kutuma mwakilishi wake ambaye ni Mkuu wa Polisi
Wilaya, Dominic Mlei na Mkuu Mpya wa Polisi wa Wilaya atakayeanza kazi
hivi karibuni, Thadeus Malingumu.

Kwa upande wake, OCD Mlei alisema ulinzi unaanza rasmi leo, kufanya
doria maeneo yanayozunguka chuo hicho na maeneo jirani, pia chuo
kijenge hosteli za kutosha na kwa kila hosteli za nje na nyumba
walizopanga wanafunzi zitakaguliwa kesho na mapungufu ya kiusalama
kwenye makazi hayo yataainishwa na wamiliki wataitwa na hosteli zote
zitatakiwa kuwa na mageti na ulinzi wa makazi hayo kuboreshwa.

Pia alitaka kuundwa kwa mara moja kwa vikundi vya ulinzi shirikishi.

Hata hivyo, mtumishi wa Chuo hicho, Mzee Muganda alishauri Kituo Kidogo cha Polisi kijengwe Kikuyu na bidii ya doria iongezwe

Source: Habari Leo Mtandaoni

Hiyo ni Tanzania the peaceful country in Africa.
Kigoma uporaji unaanza saa kumi na mbili jioni siku hizi; mitaa inatekwa, target ni maduka na vibanda vya Mpesa
 
Hapo kwenye hilo la kubakwa....kwanini wabakwe?,siyo ksbb ya nguo fupi na fashion zao za siku hizi za kutopiga underwear hivyo kutengeneza mazingira ya dhahiri kabisa? mana'ke wanafunzi wa siku hizi wa Higher Learning Institution wamezidi.
 
Anselm, na hao wanaolawitiwa je? Wanavaa nn cha kuwavutia?
 
Last edited by a moderator:
Waziri wa elimu, waziri wa ustawi wa jamii, waziri wa mambo ya ndani mnasemaje hapo?
Hamjawatuma askari wenu kwenda kuwapiga mabomu? au kwa vile hawadai hela?

Wakiandamana kudai hela mnasikiaga haraka sana na kuwazuia hata kabla hawatoka eneo la chuo!
 
Hapo kwenye hilo la kubakwa....kwanini wabakwe?,siyo ksbb ya nguo fupi na fashion zao za siku hizi za kutopiga underwear hivyo kutengeneza mazingira ya dhahiri kabisa? mana'ke wanafunzi wa siku hizi wa Higher Learning Institution wamezidi.
Very low! Unahalalisha uhalifu kwa kisingizio cha udhaifu wako?
 
Astaghafurah!! Kulawitiana tena? Hao ni watu wa wapi wasio na kinyaa??
 
Hapo kwenye hilo la kubakwa....kwanini wabakwe?,siyo ksbb ya nguo fupi na fashion zao za siku hizi za kutopiga underwear hivyo kutengeneza mazingira ya dhahiri kabisa? mana'ke wanafunzi wa siku hizi wa Higher Learning Institution wamezidi.
Anselm:focus:hiki chuo nacho kule kimekaa vibaya sana mungu wangu du!
 
Hapo kwenye hilo la kubakwa....kwanini wabakwe?,siyo ksbb ya nguo fupi na fashion zao za siku hizi za kutopiga underwear hivyo kutengeneza mazingira ya dhahiri kabisa? mana'ke wanafunzi wa siku hizi wa Higher Learning Institution wamezidi.

je na huyo mwanaume aliyelawitiwa alivaa suruali fupi eenh?
 
Hao wanafunzi nashauri wawe wanatembea kwa makundi kuanzia watatu na kuendelea la sivyo usiku ukiingia tu wawe ni watu wa ndani kabla ulinzi haujaimarishwa, mwanafunzi akibakwa au kulawitiwa sidhan kama ataingia darasani tena, pole sana wanafunzi.
 
haha akulawitiwa?afu unaulizwa inauma au?hahaa poleni wanafunzi wa chuo kikuu kwa kubakwa na kulawitiwa
 
Hapo kwenye hilo la kubakwa....kwanini wabakwe?,siyo ksbb ya nguo fupi na fashion zao za siku hizi za kutopiga underwear hivyo kutengeneza mazingira ya dhahiri kabisa? mana'ke wanafunzi wa siku hizi wa Higher Learning Institution wamezidi.

Mkuu you are one of respectable dude around, but this one takes you way down under
 
Very low! Unahalalisha uhalifu kwa kisingizio cha udhaifu wako?

Hapa mwenye udhaifu sijui ni yupi? aliyeacha mila au aliyereact baada ya mila kuachwa. Hata hivyo uharifu wa aina yoyote ni mbaya ACHENI.

We mwizi ambaye kimsingi jamii imemshindwa hadi amekuwa jambazi aina hiyo anamkuta dada sketi au suruali yuko kama uchi tu unadhani atamwacha??? skin tight, bila chupi kama wanavyosema vijana, sketi aikiinamana ****** nje, pili amkuta mkaka eti amevaa kata K, suruali magotini, jambazi alishachizi siku mingi hakuachi. Hivyo kuvaa kwa heshima kunaweza punguza mhemko wa jambazi aka-consentrate na wizi tu. Heri nusu shari kuliko shari kamili.
 
hiyo ni tanzania the peaceful country in africa.
Kigoma uporaji unaanza saa kumi na mbili jioni siku hizi; mitaa inatekwa, target ni maduka na vibanda vya mpesa
amani majumbani mwao tu,watu wamecho wananjaa,maisha hayana matumaini,hujui kesho itakuwaje!!!ni vigumu sana kupunguza ubarifu zaid vibama na changu doa.
 
Hapo kwenye hilo la kubakwa....kwanini wabakwe?,siyo ksbb ya nguo fupi na fashion zao za siku hizi za kutopiga underwear hivyo kutengeneza mazingira ya dhahiri kabisa? mana'ke wanafunzi wa siku hizi wa Higher Learning Institution wamezidi.

Wewe nawe unaongea nini? Kwahiyo aliyelawitiwa alivaa nguo fupi? Mbona mnakuwaga na negative zaidi ya positive? Ndo maana bongo maendeleo hamna maana wivu na husuda vimewajaa

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom