Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Kuna taarifa za kuaminika kuwa mda huu wanafunzi wa kitivo cha elimu UDOM wameanza mgomo kwa maandamano kuelekea utawala mkuu ili kushinikiza malipo ya fedha zao za kujikimu. Hii ni baada ya pesa kucheleweshwa sana huku ikiaminika kuwa pesa ziko chuoni tayari tangu dec.17 kwani majina waliyoletewa yana muhuri wa tarehe hiyo wa crdb(PAID-TAR,17 dec). Walio sain hata kabla ya xmas pesa hawajapata,huku wengine hata pesa ya kwanza hawajapata na utawala wanasema hautambui hilo na wengine majina yao hakuna kabisa! TUUNGANE KUTOKOMEZA UFISADI KWA KUTOOGOPA VITISHO!!