Wanafunzi Ilboru waendelea kugoma

Wanafunzi Ilboru waendelea kugoma

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
[h=2][/h]

Mulugo%2814%29.jpg

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Phillipo Mulugo

Mgomo wa wanafunzi wa Sekondari ya Ilboru, iliyopo wilayani Arumeru, kutoingia madarasani uliingia siku ya pili jana, wakishinikiza mwanafunzi mwenzao Ibrahim Kaebo wa kidato cha tatu ‘C’ aliyefukuzwa na bodi bila kupewa nafasi ya kujitetea, kurejeshwa shuleni.

Akizungumza katika ofisi za NIPASHE mjini hapa, alisema yeye ni Makamu Mwenyekiti wa chakula na bwalo, hivyo akiwa kiongozi alikuwa anakabiliwa na changamoto za chakula kuwa kibovu na wenzake kugoma kula, hivyo kama wajibu wake aliandika taarifa, jambo lililomponza kuwa anajifanya mjuaji.

Alisema alimsindikiza mwanafunzi mwenzao hospitalini, (hakumtaja jina), baada ya kuumizwa mkono kwa kuchapwa viboko na mwalimu, jambo lililopelekwa katika bodi kuwa alitaka mwalimu afukuzwe kazi.

Makosa mengine aliyataja kuwa ni kuondoka shuleni bila ruhusa, kutofanya mitihani, kudharau walimu, kuwapiga wanafunzi na kuwajeruhi, kukataa kumeza dawa, jambo ambalo alieleza kuwa siyo la kweli.

Kaebo alisema kinachomsikitisha zaidi ni kumfukuza shuleni hapo bila kumpa nafasi ya kujitetea na kwamba hajawahi kufanya kosa lolote lililosababisha apewe barua ya onyo.

Alisema baada ya kutaka apewe barua yenye kueleza makosa aliyofanya hakupewa, badala yake alipata vitisho vya kutakiwa kuondoka shuleni hapo.

“Nikiwa shuleni Mwalimu Mkuu wetu, Julius Shulla, aliita wanafunzi wenzangu mstarini na kuanza kuwaeleza sababu za kunifukuza, jambo lililowashangaza na kuamua kugoma kuingia madarasani,” alisema.
Kaebo alisema wanafunzi wanagomea mambo mengi ikiwamo tabia ya kubadilishiwa mabweni na walimu bila kuhusisha uongozi wa shule kama mtaala unavyosema.

Kasoro nyingine ni kubadilishiwa ratiba ya chakula na kulazimishwa kuchagua vyakula vya bei nafuu.

Mmoja wa viongozi wa wanafunzi shuleni hapo, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema alichotendewa mwanafunzi mwenzao siyo haki na makosa hayo siyo ya kweli, maana alikuwa mtetezi wao kama kiongozi.

Alisema hata kama alikosa shule ingempa nafasi ya kujieleza, jambo ambalo hawakubaliani nalo na wataendelea kugoma.

Wanafunzi hao wamegoma kwa kujikusanya kwenye mabweni, bila kuingia madarasani.

Waandishi walikwenda shuleni hapo kutaka kumwona Mkuu wa shule lakini alikataa kuonana nao kwa kile kilichoelezwa kwamba akihitaji kuongea na waandishi atawaita.
 
Kuna waalimu wengine ni wapuuzi sana niliwahi kumpa kichapo mwalimu kwa upuuzi kama huo wa vyakula vibovu. wanawafanya wanafunzi kama misukule wawalishe kila takataka.
 
Mishule ya Serikali imechoka kama magari ya 109 landrover vyakula ovyo kila ki2 ovyo
 
though mimi. ndiye niliyeanzisha vuguvugu la mabadiliko tangu mwaka juz shuleni hapo nawashauri madogo waache mgomo bali wajikite kusoma coz kitakachowakuta kwa mgomo huu sijui 2.....
 
though mimi. ndiye niliyeanzisha vuguvugu la mabadiliko tangu mwaka juz shuleni hapo nawashauri madogo waache mgomo bali wajikite kusoma coz kitakachowakuta kwa mgomo huu sijui 2.....

Mmmmmmh. Pole sana,Ilboru na migomo hawajaanza Juzi kaka.
 
Mmmmmmh. Pole sana,Ilboru na migomo hawajaanza Juzi kaka.

kwa taarifa yako tangu aondoke Julius Matiko na kuingia mutabuzi viongozi walkua masnitch mpaka mwaka juz ndio vijana wa m4c waliposhika dola mambo yakaanza kwenda sawa na hatimaye kumng'oa mutabuzi ndio kaingia shulla
 
Binna?
 
namfaham xana shulla alkua mkuu wa tosamaganga kabla ya hapo..Popote alipo huyo bwana hapakos matatzo--anauwezo mzur wa kuwaunganisha walmu lakn huwa anawakandamz xana wanafunz.
 
though mimi. ndiye niliyeanzisha vuguvugu la mabadiliko tangu mwaka juz shuleni hapo nawashauri madogo waache mgomo bali wajikite kusoma coz kitakachowakuta kwa mgomo huu sijui 2.....

Mkuu vuguvugu ya mabadiliko haijaanza mwaka juzi. Tumeanzisha mgomo toka 2001 pale, then 2005 etc. Tuliking'oa kisiki cha mpingo-Kitemango, then akaja Kwayu. Kitemango alikuwa na mizizi mpaka Ikulu but akatoka. Kiujumla Kwayu alikuwa vizuri kutatua migogoro. Thereafter ndio wakaja hao milugo wenu mkuu.
 
Kwa akili yenu ya kdato cha 6 au cha 4,huo mgomo unataratbu zote msing za kufuatwa? au mmemamua tu! na km hakuna ruhusa ya kugoma bora mtatue kwa njia zngne!KUMBUKA HI NI SERIKALI YA TANZANIA NA SI USA! soma geog paper2, hebu tulieni, HP wajibika!
 
Mkuu vuguvugu ya mabadiliko haijaanza mwaka juzi. Tumeanzisha mgomo toka 2001 pale, then 2005 etc. Tuliking'oa kisiki cha mpingo-Kitemango, then akaja Kwayu. Kitemango alikuwa na mizizi mpaka Ikulu but akatoka. Kiujumla Kwayu alikuwa vizuri kutatua migogoro. Thereafter ndio wakaja hao milugo wenu mkuu.

Bora ulikuwepo eti yeye ndio chachu ya mabadiliko Ilboru,vijana bwana.
 
wewe Binnah humjui vizur na sikulaumu kwa kutokumjua bila shaka umemjua kuanzia 2011 hivi!

Sihitaji kumfahamu mpuuzi kama huyo,nimesikia tu taarifa zinazomhusu. Ilboru nimepita wakati wewe unakazana ukasome pale.
 
Shulla mm nimemjua tangu npo Tosamaganga ndo huyo huyo aliyesababisha Mgomo 2011 yule mzee ana spirt chafu xana anakandamiza wanafunz huku akiwatenga na Walimu waoo! Nahc yule mzee ashushwe cheo....
 
Oh! Poleni wanafunzi. Hii inanikumbusha wakati nikiwa mwanafunzi Ilboru,tuligoma kula maana chakula hakikuwa na chumvi, na maharagwe yalikuwa na wadudu. Headmaster Mtui akasema kama hatuli tuishie majumbani kwetu. Wanafunzi walikasirika wakaenda nyumbani kwa headmaster na kuiponda gari yake kwa mawe. Huwa nikikumbuka hilo tukio nabaki kucheka tu.
 
Back
Top Bottom