hassan yahaya
Member
- Aug 27, 2022
- 35
- 37
Hii ni kwaajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wametoka katika familia duni. Umezuka mtindo kwamba wanafunzi wengi waliotoka familia zenye hali duni na kwenda vyuo vikuu kubadilika na kujisahaulisha hali halisi ya nyumbani kwao.
Umetoka nyumbani hali ni dhaifu mnaishi nyumba ya nyasi, mama anapikia jiko la kuni, wadogo zako wanaenda shule sare zao zina viraka vitupu, baba yako analima shamba lake kisha anafanya kazi ya kibarua ili apate pesa akulupie wewe na akidhi mahitaji ya familia
Leo hii wewe umekuja chuo kikuu unasahau ulipotoka unaanza kuishi kama kwenu ni tajiri, unamiliki simu ya iphone, unanunua kitanda cha laki mbili na nusu, unajifunza kunywa pombe, unaenda kumbi za starehe ili tu usionekane kuwa kwenu masikini, dear brother/sister hiyo hela si bora umtumie mama yako huko kijijini imsaidie.
Unafika chuo unaacha kusoma kwa kuwafata wanafunzi wenzio ambao wametoka familia ambazo ni tajiri na unasahau kama kwenu ukoo mzima wewe ni wakwanza kusoma na wote wanadhani kwamba ukifanikiwa utakuja kuwasaidia lakini wewe unasahau na kuanza tabia za ajabu mwisho unapoteza CV unafukuzwa chuo unarudi nyumabni unalia.
Hebu tubadilike ishi kulingana na hali ya familia yako chuo umekuja kusoma sio kustarehe tumia simu ya kawaida tu usitake kumiliki vitu vya bei ghali kwa pesa unayolipiwa na wazazi wako, kuna mtu atasema hii pesa napokea boom sio ya mzazi hii, my dear ni kweli ila hiyo pesa kama ungemtumia mama yako angekushukuru na kukuombea dua nawe upate baraka zake.
Tujitambue wanafunzi wenzangu kwetu wanatutegemea