opportunist2012
Member
- Feb 8, 2012
- 92
- 9
Natoa rai kwa wote mliofeli mtihani wa kidato cha nne kuwa makini na wanasiasa wanaowachonganisha na serikali yetu tukufu ya Tanzania. Wanasiasa hao wamekuwa wakiwafanya muichukie serikali yenu kwa kutoa kauli mbalimbali mara baada ya kutangazwa matokeo ya kidato cha nne. Wanaweza kuwatumia kwa masilahi yao kisiasa.....kuna uwezekano mkubwa wakawaambia muandamane kupinga matokeo ya kidato cha nne. Kamwe msidanganyike. watawatumbukiza katika matatizo makubwa.
Ninajua wengi wenu mmepokea matokeo kwa masikitiko, hizi kauli za wanasiasa hazina mashiko...eti matokeo ya kidato cha nne yamekuwa mabaya kwa sababu zifuatazo hasa katika shule za serikali ;uhaba wa walimu, maslahi duni ya walimu, ukosefu wa maabara na zana za kufundishia, walimu kukata tamaa....sikubaliani na sababu hizi moja kwa moja...iweje shule za private kama Green Acres, Jitegemee, Makongo, Kenton zifanye vibaya ? kama sababu ndo hizo ?
Shule hizi zina kila kitu ;walimu wa kutosha wenye kulipwa vizuri, maabara na zana za kufundishia za kutosha, walimu wenye kujituma...na bado matokeo mabaya, ziro kibao...KUNA SABABU NYINGINE ZA MATOKEO MABAYA...Serikali haipaswi kulaumiwa...tusiwafanye walioshindwa mtihani waichukie serikali. Serikali inafanya kila juhudi kuboresha elimu ya nchi yetu...
Tusiyageuze matokeo ya kidato cha nne kama jukwaa la siasa uchwara.....naomba kuwasilisha.