Wanafunzi sekondari watengewa 25,000/-

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,112
Reaction score
4,540
KATIKA kipindi cha mwaka 2012/13, serikali imetangaza kuwa kila mwanafunzi katika shule za sekondari za serikali nchini, ametengewa kiasi cha sh 25,000 kwa ajili ya huduma mbalimbali wanazopatiwa kutoka serikali.

Akijibu swali bungeni jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alisema kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya upatikanaji wa vitendea kazi. Mulugo alisema kuwa, fedha hizo ni ongezeko la sh 4,000 kwa kila mwanafunzi kutoka bajeti ya mwaka uliopita (2011/12) ambapo kila mwanafunzi alitengewa kiasi cha sh 21,000.

Alikuwa akijibu swali la Joseph Selasini (CCM) aliyetaka kujua iwapo serikali itakuwa tayari kusaidia nguvu za wananchi wa Rombo kwa kuwapatia maabara, maktaba, walimu wa kutosha na vitendea kazi baada ya wananchi kujenga majengo ya kutosha kwa ajili ya shule hizo.
Selasini alihoji iwapo serikali itakuwa tayari kushirikiana na wananchi wa Rombo kujenga Chuo cha Ufundi (VETA) ili iwaweshe wanafunzi wanaomaliza kidato cha 5 na 6 wajiendeleze.

Naibu Waziri alisema katika mwaka wa fedha 2012/12, serikali ina mpango wa kuboresha miundombinu ya shule 264 nchi nzima ambazo ni sawa na shule mbili kwa kila halmashauri. Kwa mujibu wa Mulugo, serikali inatekeleza sera ya kushirikiana na sekta binafsi na wananchi katika kufanikisha mipango ya maendeleo, hivyo akawataka wananchi wa Wilaya ya Rombo kuwa huru kujenga Chuo cha VETA na serikali itawaunga mkono.
Tanzania Daima
 
Joseph Selasini wa Rombo ni Mbunge kwa tiketi ya CHADEMA na siyo CCM kama ulivyoandika; au umeisha asilika na ma-rangi ya Njano na Kijani?????
 
"Wanafunzi sekondari watengewa 25,000/-"ukisoma kwa haraka kichwa kinatia raha nenda sasa kwenye utekelezaji na matumizi hakika utajuta ikiwa mwanao yupo kwenye shule hizo za kata!
 
Inamaana wataanza kunywa chai mkate asubuhi, ugali na mnoga 3 mchana na wali jioni? Ata sitaki kuliongelea sana maana nimetoka huko huko...
 
"Wanafunzi sekondari watengewa 25,000/-"ukisoma kwa haraka kichwa kinatia raha nenda sasa kwenye utekelezaji na matumizi hakika utajuta ikiwa mwanao yupo kwenye shule hizo za kata!

Ufisadi mtupu! Huko shule za msingi tangu 2002 UN kupitia nadhani UNICEF inatoa US $10 (kama Shs 15,000/-)kwa kila mwanafunzi kwa mwaka(hela hiyo wenyewe wanaiita "CAPITATION"). Kaulize, hadi inamfikia mwanafunzi inabaki Shs.600/- kwa mwaka. Hiyo hela inaliwa wizarani, inaliwa mkoani, inaliwa wilayani hadi kuja kufika ni shilingi mia sita badala ya takriban Shs.15,000/-. HIYO NDIYO SERIKALI YA CCM.
 

Waziri Mulugo anatakiwa alieleze taifa ni kiasi gani cha fedha kwa kila mwanafunzi wa sekondari kilipelekwa shuleni kwa mwaka wa fedha uliopita. Hizi ni ngonjera. Nendeni katika hizo shule ndiyo mtajua hali halisi ikoje.
 

da hapo penye red cjaelewa ana maana gani?
 
Waziri Mulugo anatakiwa alieleze taifa ni kiasi gani cha fedha kwa kila mwanafunzi wa sekondari kilipelekwa shuleni kwa mwaka wa fedha uliopita. Hizi ni ngonjera. Nendeni katika hizo shule ndiyo mtajua hali halisi ikoje.

Nadhani unaongea tu, umefuatilia na kuhakikisha hazipelekwi? Kwa kutekeleza hili CCM nawasifu, hizi hela zinafika ingawa ucheleweshwa. Kwa hili wakati nafanya Review za utekelezaji wa sera za elimu nishangazwa kukuta hela zikipelekwa kila mwaka. Ukiona hakuna utekelezaji bana mkuu wa shule ujue anakozipeleka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…