KATIKA kipindi cha mwaka 2012/13, serikali imetangaza kuwa kila mwanafunzi katika shule za sekondari za serikali nchini, ametengewa kiasi cha sh 25,000 kwa ajili ya huduma mbalimbali wanazopatiwa kutoka serikali.
Akijibu swali bungeni jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo alisema kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya upatikanaji wa vitendea kazi. Mulugo alisema kuwa, fedha hizo ni ongezeko la sh 4,000 kwa kila mwanafunzi kutoka bajeti ya mwaka uliopita (2011/12) ambapo kila mwanafunzi alitengewa kiasi cha sh 21,000.
Alikuwa akijibu swali la Joseph Selasini (CCM) aliyetaka kujua iwapo serikali itakuwa tayari kusaidia nguvu za wananchi wa Rombo kwa kuwapatia maabara, maktaba, walimu wa kutosha na vitendea kazi baada ya wananchi kujenga majengo ya kutosha kwa ajili ya shule hizo.
Selasini alihoji iwapo serikali itakuwa tayari kushirikiana na wananchi wa Rombo kujenga Chuo cha Ufundi (VETA) ili iwaweshe wanafunzi wanaomaliza kidato cha 5 na 6 wajiendeleze.
Naibu Waziri alisema katika mwaka wa fedha 2012/12, serikali ina mpango wa kuboresha miundombinu ya shule 264 nchi nzima ambazo ni sawa na shule mbili kwa kila halmashauri. Kwa mujibu wa Mulugo, serikali inatekeleza sera ya kushirikiana na sekta binafsi na wananchi katika kufanikisha mipango ya maendeleo, hivyo akawataka wananchi wa Wilaya ya Rombo kuwa huru kujenga Chuo cha VETA na serikali itawaunga mkono.
Tanzania Daima