KERO Wanafunzi tunadai fedha za refund lakini Chuo cha St. John's University of Tanzania kinatuzungusha tu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi Wanafunzi wa St. John's University of Tanzania cha Dodoma tunakidai chuo hela ambazo tulilipa kabla hatujalipiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), tumeandika barua nyingi sana kuomba waturudishie fedha zetu (refund).

Wazazi wengine walikuwa wanakopa ili watulipie ada na michango mingine wakiamini zitarejeshwa na kuingizwa kwenye matumizi ama ya mhusika au ya Mwanafunzi lakini chuo kinatuzungusha na kugoma kuturudishia fedha zetu na kutuwekea masharti magumu sana.

Wanafunzi wengi tunaodai ni wa ngazi tofauti, mfano sisi ni Wanafunzi wa Mwaka wa Tatu, madai tunayodai ni yale ambayo tulilipa wakati tunaanza Mwaka wa Kwanza Mwaka wa mazomo 2021/22.

Tulilipa zaidi ya Shilingi Milioni 1 (malipo yanategemea na aina ya kozi), hadi sasa ni mwaka wa Tatu hatujalipwa, tunazungushwa tu.

Kuna wachache ambao wamelipwa lakini kwa kucheza michezo na watu wa Idara ya fedha, wanaambiwa kwa kuwa hujarejeshewa fedha zako, mtafute mtu ambaye hajalipa ada, unampeleka kwake, wanachofanya ile amount ambayo mtu unadai kwa kuwa inaonekana kwenye mfumo wanaihamishia kwa mhusika mwingine kisha yule anayelipa anatoa fedha cash kwa makubaliano kwamba mtu wa Idara ya Fedha naye anapata chochote.

Sisi ambao hatutaki michezo ya aina hiyo wanatukazia na tunaendelea kulallamika mpaka sasa.

Kinachouma zaidi ni kuwa wapo ambao wanamaliza chuo mwaka huu na hawajalipwa, hiyo inamaanisha watahitimu bila kurejeshewa fedha zao.
 
Wazazi walishalipa milioni moja ada ilitakiwa baada ya pesa ya bodies ya mikopo kuingia mwanafunzi husika ilitakiwa uwarudishie wazazi wako milioni moja yao waliolipa ada na usiendelee kusumbua chuo
 
Ada inayolipwa na bodi haiingii kwenye account ya mwanafunzi. Ada inaingia kwenye account ya chuo, mwanafunzi anasaini tuu. Hivyo Chuo kimechukua Ada mara 2 kwa mwanafunzi mmoja.
 
Sisi Wanafunzi wa St. John's University of Tanzania cha Dodoma tunakidai chuo hela ambazo tulilipa kabla hatujalipiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), tumeandika barua nyingi sana kuomba waturudishie fedha zetu (refund).

Wazazi wengine walikuwa wanakopa ili watulipie ada na michango mingine wakiamini zitarejeshwa na kuingizwa kwenye matumizi ama ya mhusika au ya Mwanafunzi lakini chuo kinatuzungusha na kugoma kuturudishia fedha zetu na kutuwekea masharti magumu sana.

Wanafunzi wengi tunaodai ni wa ngazi tofauti, mfano sisi ni Wanafunzi wa Mwaka wa Tatu, madai tunayodai ni yale ambayo tulilipa wakati tunaanza Mwaka wa Kwanza Mwaka wa mazomo 2021/22.

Tulilipa zaidi ya Shilingi Milioni 1 (malipo yanategemea na aina ya kozi), hadi sasa ni mwaka wa Tatu hatujalipwa, tunazungushwa tu.

Kuna wachache ambao wamelipwa lakini kwa kucheza michezo na watu wa Idara ya fedha, wanaambiwa kwa kuwa hujarejeshewa fedha zako, mtafute mtu ambaye hajalipa ada, unampeleka kwake, wanachofanya ile amount ambayo mtu unadai kwa kuwa inaonekana kwenye mfumo wanaihamishia kwa mhusika mwingine kisha yule anayelipa anatoa fedha cash kwa makubaliano kwamba mtu wa Idara ya Fedha naye anapata chochote.

Sisi ambao hatutaki michezo ya aina hiyo wanatukazia na tunaendelea kulallamika mpaka sasa.

Kinachouma zaidi ni kuwa wapo ambao wanamaliza chuo mwaka huu na hawajalipwa, hiyo inamaanisha watahitimu bila kurejeshewa fedha zao.
Miaka yote huwa wanasumbua sana, hela ikiingia kwenye account ya chuo kuitoa ni kazi. Hapo ungekua unakaa hostel then wanakukata kwenye hiyo ada. Pia direct charges za chuo hulipi, inakatwa hukohuko. Mngemalizana kirahisi
 
Mimi ni muhitimu wa Chuo Kikuu St.John's au St.John's University of Tanzania, tumehitimu Mwaka huu 2024 lakini Mwaka 2022 kuna fedha ambazo tulizidisha kwenye malipo ya Ada.

Kutokana na hali hiyo, mikopo ambayo tulikuwa tunapata kutoka Bodi ya Mkopo ilipoingizwa kwenye akaunti ya Chuo baada ya sisi kulipa ada awali, tukaahidiwa kurejeshewa malipo hayo yaliyozidi.

Wapo ambao wanadai hadi Shilingi Milioni 2, hapo kati tuliandikishwa barua kama mara mbili hivi ili wachukue taarifa zetu watulipe lakini mpaka sasa kimya.

Kila tukiulizia tunaambiwa watalipa, mpaka sasa tumehitimu na tupo nyumbani wanasema watatulipa, lini au ndio tuandike maumivu?

Tukimuuliza Rais wa Wanafunzi anatuambia tutalipwa tu, inauma sana. Turudishiwe hela zetu.
 
Back
Top Bottom