Wanafunzi udom watamani chuo kifungwe

Wanafunzi udom watamani chuo kifungwe

Posho City

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2012
Posts
648
Reaction score
418
Katika hali ya kushangaza wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wanatamani chuo kifungwe ili angalau wende kwao wapate kufurahi utu wao.Hii ni kutokana na sababu kuwa serikali kupitia bodi ya mikopo imegoma kuwapa hela za kujikimu wanafunzi hao.Hela hiyo walitakiwa kuipata tarehe 3.5.2012 lakini hadi leo hawajui lini inapatikana.Wiki moja iliyopita uongozi wa chuo uliweka matangazo kuwa bodi ya mikopo haijatuma hela na hawajui lini itatumwa.Hali hiyo inakuja wakati kukiwa na taarifa za hazina ya serikali kuishiwa hela.Hali ni mbaya hasa huku kitivo cha elimu wanafunzi wanashindia viazi vitamu kati ya viwili na kimoja
 
Kikwete alinunuliwa form na wana udom,,,,,mkapa ndo vc wao sasa tatizo liko wapi
 
hivi wale wanavyuo walioandamana kuhusu sijui nini nini sisiemu inamaana wao boom walipata au ndio walewale walioenda kwa majina ya babazao na kughushi mitihani? Inasikitisha sana kuona wanavyuo wanateseka na njaa,sijui tutakua na wasomi wa aina gani kwa njaa hii wanayoteseka nayo.ccm wasitafute mchawi 2015
 
Poleni sana vijana ila nawashauri uiteni uongozi wa chuo muwaeleze hali halisi ili kama hakuna njia mbadala mfunge na hivi hakuna wajasi sijui pale social watu wanaishije.kwa ujumla maisha ya chuo bila hela ni mateso sana na kwaambayd hajapitia hawezi kutambua na hapa ndipo dada zetu wanapo angukia kwenye midomo ya mafataki ili wajikimu serikali na uongozi wa vyuo husika fungeni vyuo kama hakuna fedha muokoe taifa kutoka kwenye uwezekano wa kupata matatizo ya kiafya kwa wanafunzi husika kama vile Hiv na magonjwa ya zinaa kwa kinadada na pia vidonda vya tumbo ambayo yanahatarisha uwajibikaji wa wanafunzi husika ukizingatia mwanafunzi hawezi kusoma huku hana kitu tumboni itakuwa ni kuumizana
 
Poleni bandugu. Once upon time, way back in history chakula campus was no mgogoro. We used to enjoy 3 course meal fit for a king. Breakfast served six to eight am, lunch eleven to two pm, supper six to eight pm. Oh how we used to "rewind" on days chicken(which we foundly called flamingos) was served. We would have an early lunch at eleven and another late one just before two pm finish off with coffee and jelly. Cost sharing imekuwa shida tupu.
 
Pole sana madogo. Kuanzia tarehe 3 hadi 18 ni muda mrefu sana kwa maisha ya chuo! Tafuteni ukweli zaidi kama serikali haina hela bora chuo kifungwe.
 
siku nyingine msimnunulie mgombea fomu, poleni
 
Back
Top Bottom