Kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambao wanadhaminiwa na bodi ya mikopo huku hatma ya wanafunzi hao kupata fedha zao za kujikimu kwa awamu ya nne ikiwa haijulikani hatimaye wanafunzi wa chuo kikuu dar es salaam UDSM wameamua kuanza rasmi mgomo na maandamano yasiyokoma kesho Jumatatu ya tar. 5 Mei.
Maandamano hayo makubwa ya kushinikiza kupata malipo yao[boom] kwa awamu ya nne yanatarajia kuanza kesho saa moja kamili asubuhi katika eneo la chuo hicho linalojulikana kama REVOLUTION SQUARE na kisha kuelekea barabara ya Ubungo na kumalizikia katika makao makuu ya bodi ya mikopo-HESLB..
Tayari mabango yenye jumbe mbalimbali yanaandaliwa katika hostel za mabibo na main campus ili kuweza kutumika siku ya kesho..
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA.. "SOLIDARITY FOREVER"