nafikiri tatizo lao si chakula bali ni hela! College wanayogoma asilimia kubwa ni wale ambao wanapewa mkopo wa ada kwa % hivyo wengi wao hawana mkopo wa asilimia mia moja. Kwa hiyo vyuo wanapodai ada wanafunzi wanachofanya ni kuchukua sehemu ya hela ya chakula na kulipa ada hivyo wanakuwa hawana hela ya kutosha ya chakula. Tangazo la chuo linasema kuwa wanakopeshwa na hela hizo watalazimika kuzirudisha semester ijayo hivyo hata wakati ujao tatizo litajirudia. Mbona madai ya hela ya kujikimu hayakuwa miongoni mwa madai ya Inginiazi?