Wanafunzi nao wanatakiwa kueleza ukweli ni kitu gani kinaendelea kati yao na board. Suala lenyewe lilivyo ni kama ifuatavyo. Mwanzoni mwa muhula wa masomo, board ya mikopo ilitoa fedha pungufu kwa wanachuo (badala ya kuwapa pesa ya muhula mzima, ili wapatia ya nusu muhula (Miezi miwili, Sep/oct, Oct/Nov)). Wanafunzi wengi walilalamika sana maana wengi wao huwa wanatumia sehemu ya hiyo pesa kulipia hata hizo % ambazo hawalipiwi na board kwenye ada. Wakati board wanajiandaa kuwapatia pesa iliyokuwa imesalia, tayari wanachuo walikuwa katika hekaheka za mgomo. Kabla ya tangazo la kuvifunga vyuo halijatoka board ya mikopo ilipost hela tayari kwa baadhi wa wanachuo wa UDSM. Kwa DUCE karibia wanachuo wote walipewa pesa. Sina taarifa ya vyuo vingine. Hao walipewa kiasi gani? Walipewa pesa ya kumalizia miezi miwili ya mwisho ya muhula wa kwanza (Sh. 300,000 ambayo ilitakiwa iwe for Nov/Dec, Dec/Jan) na pesa ya kuanzia muhula wa pili (ya miezi miwili Sh 300,000 ambayo wangeitumia kwa mwezi Feb/March, march/April). Hivyo basi wakati chuo kinafungwa wale waliokwisha kupata hela walipokuwa wanaondoka walikuwa na jumla ya sh. 720,000 kwenye account zao. Walizitumiaje wakiwa nyumbani baada ya chuo kufungwa na baada ya chuo kufunguliwa ili kumalizia muhula wa kwanza tuwaulize wao.
Tukija kwa wale ambao hawakuwekewa hela kwenye account zao wakati vyuo vinafungwa. Wengi wao waliwekewa wakati vyuo vilipofunguliwa mwezi january na february. Na wao walipewa pesa kama wenzao jumla sh. 600,000 ikiwa na maana kuwa sehemu ya hiyo pesa ni kwa ajili ya miezi miwili ya mwisho ya muhula wa pili (sh. 300,000 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya Feb/March, March/April) na nyingine ni nyingine ni kwa ajili ya miezi miwili ya mwanzo ya muhula wa pili (sh. 300,000, April/May, May/June). Nina mdogo wangu na mtoto wa uncle wanasoma UDSM ambao niliwashauri wanipatie pesa niwahifadhie ambazo nilikuwa kwa za muhula wa pili (300,000). Hili nililifanya kutokana na experience yangu nilipokuwa mwananchuo. Nilishuhudia wananchuo wengi wakipata shida kutokana na matumizi mabovu. Akina dogo walikuwa waelewa walinipatia zile pesa (jumla 600,000). Chuo kilipofunguliwa mid April niliwapatia pesa zao zote.
Wanachuo wengi walikuwa wameshalipwa pesa kwa ajili ya miezi miwili ya mwanzo ya muhula wa pili (April/May, and May/June). Kama wanaidai board, basi ni ile pesa sh. 300,000 ambazo ni kwa aliji ya mwezi June/July, July/Aug. Na kwa kawaida ya board hiyo pesa ingetolewa kwenye tar. 10 mwezi wa sita. Kwa mwanachuo ambaye anadai sh. 600,000 mpaka sasa, huyo hata akigoma mi namuunga mkono maana atakuwa anaonewa kwa kiasi kikubwa. Wengine waliobaki watafute tu njia nzuri ya kunegotiate na board kwa sababu hawana sababu ya msingi ya kugoma maana muda wa kupewa pesa yao iliyobaki haujafika.
Mambo niliyo observe ni kuwa, Board hawana utaratibu mzuri wa kutoa pesa, na wanachuo wengi nao hawana mpango mzuri wa kutumia pesa.