KERO Wanafunzi wa Beroya Mission Sec School wanapigwa kwa kutumia mabomba

KERO Wanafunzi wa Beroya Mission Sec School wanapigwa kwa kutumia mabomba

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Shule ya BEROYA MISSION SECONDARY SCHOOL iliyopo mkoa wa Pwani, Bagamoyo kijiji cha matimbwa ilianza kuchapa wanafunzi mwishoni mwa mwaka 2023 kwa kutumia mabomba ya maji.

Watoto wanakuwa na hofu inawa affect kisaikolojia muda wote kuwaza kuchapwa kisa ufaulu uwe mzuri sana (HAISAIDII MAANA DIVISION 4 ZIPO matokeo ya form 2) au makosa madogo madogo ya jumla .

Walimu wengine huchapa fimbo nyingi au kuwapiga vichwani,migongoni, makofi,kufinywa matiti.

Pia.. kuwapa watoto viwembe wanyoane wanajikatakata ni hatari wanaweza kuambikizana magonjwa au vidonda kupata bacteria na kuleta madhara.

Mtoto hajawahi tumia wembe pre form one au form one anakutana nao BEROYA MISSION SECONDARY SCHOOL na ni lazima kunyoana( wengine ni 12 years old au hata chini ya hapo)

Wazazi tuambiwe kabla hawajapokea watoto kuwa watapewa viwembe wanyoane.

Wazazi wengine huamua kuhamisha watoto wao wakiona vipigo vimezidi maana watoto hurudi likizo na maalama mengi miilini ya fimbo na mabomba,alama zingine zimekuwa sugu na kuweka michoro ya fimbo.

Ahsanteni.

SERIKALI ILIANGALIE HILI,
 
Back
Top Bottom