carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, SSP Virginia Sodoka, amewaonya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustino cha Tanzania (SAUT) dhidi ya kujihusisha na vitendo vya uchochezi vinavyoweza kusababisha vurugu na kuvuruga amani, akiwataka kuelekeza nguvu zao katika masomo.
Sodoka alitoa onyo hilo wakati wa utoaji wa elimu ya ulinzi na usalama kwa wanafunzi hao jijini Mwanza, akisisitiza kuwa lengo kuu la kujiunga na chuo ni kupata elimu na kujiandaa kwa maisha ya baadaye.
Alisema baadhi ya wanafunzi wanapofika vyuoni husahau malengo yaliyowaleta na kuanza kujihusisha na shughuli zinazoweza kuwavuruga katika masomo, hali inayoweza kuathiri maendeleo yao ya kitaaluma.
“Wakati huu nyinyi ni wanafunzi na jukumu lenu kubwa ni kusoma. Muda wa kufanya siasa utafika, mtakapomaliza masomo yenu mtaweza kuamua kufanya nini katika maisha yenu. Kwa sasa zingatieni kile kilichowaleta chuoni na epukeni vitendo vya uchochezi vinavyoweza kuleta vurugu na kuhatarisha amani,” alisema.
Aidha, aliwataka kuzingatia sheria na kanuni za chuo pamoja na sheria za nchi, akisisitiza umuhimu wa kutatua changamoto zinazojitokeza kwa njia zinazokubalika badala ya kuchukua hatua zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Katika hatua nyingine, aliwaonya wanafunzi dhidi ya kujihusisha na wizi, uporaji, ulevi uliopitiliza, matumizi ya dawa za kulevya na ukahaba, akieleza kuwa vitendo hivyo vinaweza kuvuruga masomo yao na kuwaingiza katika matatizo ya kisheria.
Chanzo : Saut digital