Wanafunzi wa chuo kikuu wapewa kichapo kikali baada ya kunaswa wakijiuza

Wanafunzi wa chuo kikuu wapewa kichapo kikali baada ya kunaswa wakijiuza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
[h=3][/h]





WAREMBO watatu wanaodaiwa kuwa ni madenti wa chuo kikuu kimoja jijini Dar, waliojitambulisha kwa jina mojamoja, Rachel, Neema na Suzan, wamekumbana na balaa zito baada ya kupokea kibano cha kutosha...

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, usiku wa saa 8:00, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo madenti hao walipokea kichapo kikali kutoka kwa Polisi Jamii.

Warembo hao walifikwa na kasheshe hilo baada ya kugeuka kero kwenye geti la kigogo mmoja kwa kuwa walionywa mara kadhaa kuacha kupanga foleni katika eneo hilo na kujihusisha na vitendo vya ngono.







“Unajua walikuwa kero sana. Yaani asubuhi kukicha utakuta mipira ya kiume imetapakaa kila sehemu. Mbaya zaidi utakuta watoto wakicheza mchana wanaokota hiyo mipira ya kiume na kupuliza kama puto,” alisema shuhuda mmoja aliyeamshwa na makelele ya warembo hao wakati wakila kibano.

Aliendelea: “Unajua wakikaa hapa ni hatari tupu kwani wanaume wanaokuja kuwafuata wanaweza wakatudhuru kwa sababu hatuwajui.”


Katika tukio hilo, walinzi hao wakiwa kwenye doria, walipokea malalamiko kwa mara 1000, kutoka kwa kigogo huyo akiomba msaada wa kuwaondoa warembo hao getini kwake wanaodaiwa kujiuza eneo hilo.



Habari nyingine zilieleza kuwa wadada hao wamekuwa wakiweka mitego yao nje ya nyumba hiyo ikidaiwa kwamba lengo ni kumnasa kigogo huyo ili kumuuzia biashara yao kwa kuwa ni ‘mkataji’ mzuri wa mkwanja.


Mbali na hilo, pia ilidaiwa kuwa wanaume wapenda ngono rejareja na hatarishi huwafuata eneo hilo kupata huduma yao.




Ilidaiwa kuwa walinzi hao walielezwa kuwa katika kukuza biashara hiyo haramu, warembo hao wamekuwa wakiwabugudhi wakazi wa eneo hilo hadi kufikia hatua ya kuwagongea madirishani na kusimamisha magari hovyo


Huku wakijua wamepata wateja, kundi la kinadada hao wakiwa na vinguo vya kimitego na wengine kujifunua na kubaki nusu utupu ili kuwaonesha wanausalama hao nyeti zao wakijua ni wateja ndipo wakakutwa na kasheshe hilo.


Wanausalama hao, bila kuchelewa waliwazingira warembo hao na kuwanasa kisha kuwapa kibano lakini katika purukushani hiyo wengine walifanikiwa kupata upenyo na kuchoropoka.


Katika kibano hicho, makelele ya warembo hao yalisababisha watu kuamka na kufunga mtaa.


Kutokana na timbwili hilo la akina dada hao kuwa zito, iliwabidi polisi hao jamii watumie nguvu ya ziada kuwatuliza kabla ya kuwapeleka mbele ya sheria.

Baada ya warembo hao kudakwa, walipakizwa kwenye Bajaj na kupelekwa kituo cha polisi ili wafikishwe mahakamani.




WANAFUNZI WA CHUO KIKUU WAPEWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUNASWA WAKIJIUZA - MPEKUZI
 
Mungu atunusuru jamani, napata uchungu pale napofikiria kama angukuwa ni binti yangu au dada yangu au pengine jirani yangu.
Nashindwa kusema tatizo linalo wasukuma wanachuo kufanya hivo kwa sababu nikisema ni umasikini kuna watu watasema mbona wengine wanauwezo lakini wanafanya hivo.
Na nikisema ni tamaa za mwili au mapepo kuna watu watasema kuna wengine maisha ni magumu sana ndo maana wanalazimika kufanya huo mchezo.
HAKIKA MKONO WA MUNGU UNAHITAJIKA KATIKA KUYAMALIZA HAYA.
 
Chuo gani? Au jina ni siri hapa? je walikuwa na madesa ili kubaini kuwa ni madent?
 
Naelewa kero inayoweza kutokana na pilikapilika za hao wadada lakini hiyo ya kujitwalia mamlaka ya kuwapiga haijakaa sawa.

Hao polisi jamii wanatambuliwa kisheria? Kama wanatambuliwa, ni sheria ipi inayowatambua?

Na mamlaka yao yanaanzia na kuishia wapi?

Manake naona walichokifanya ni 'assault' ambayo ni uvunjifu wa sheria.
 
Polisi jamii ndio uchuro gani?

Ikiwa polisi na uniform zake juu haruhusiki kumpiga raia, hao polisi jamii wamepata wapi mamlaka hiyo?
 
Kwa wale mlioko nje ya Tz na hamjua police-jamii ni kitu gani, hawa ni vibaka wengine ambao nao wamekubaliwa wagange njaa kwa kupitia migongo ya serikali za mitaa. Hawa hukamata watu na kuwadai faini kubwa ili nao waendelee kuendesha maisha ktk jiji hili tukutu of this semi-anarchy bongoland/
 
Pole yao waliochezea kichapo, kama wapo wenye mchezo huo watapunguza kasi kama sio kuacha kabisa.
 
Mi nahisi haya yote yanasababishwa na serikali legelege ya jk na uongozi wake wote!
Kama wanafunzi hawapewi mikopo wao wafanyaje jamani?

Hayo yote yanasababishwa na ukapa wa Tsh.
 
Naelewa kero inayoweza kutokana na pilikapilika za hao wadada lakini hiyo ya kujitwalia mamlaka ya kuwapiga haijakaa sawa.

Hao polisi jamii wanatambuliwa kisheria? Kama wanatambuliwa, ni sheria ipi inayowatambua?

Na mamlaka yao yanaanzia na kuishia wapi?

Manake naona walichokifanya ni 'assault' ambayo ni uvunjifu wa sheria.

hao polisi jamii wenyewe hawaaminiki hata chembe...hapo labda nao waliomba huduma bure wakanyimwa ndio wakawapiga...
 
Polisi jamii wezi tu .. Unampiga mtu kwa minajili gani? Si waende kimara huko wakakutane na mabomu tuone kama watasogeza pua zao
 
Hii habari jan niliona katika gazeti moja la udaku lakini sikuisoma kwa makini hapa sasa nimeelewa kinachoendelewa
 
Naelewa kero inayoweza kutokana na pilikapilika za hao wadada lakini hiyo ya kujitwalia mamlaka ya kuwapiga haijakaa sawa.

Hao polisi jamii wanatambuliwa kisheria? Kama wanatambuliwa, ni sheria ipi inayowatambua?

Na mamlaka yao yanaanzia na kuishia wapi?

Manake naona walichokifanya ni 'assault' ambayo ni uvunjifu wa sheria.

Mkuu hata kama hao polisi jamii wangalikuwa wanatambuliwa kisheria bado swala la kujichukulia sheria mkononi sio sahihi! Katika utawala wa kweli wa sheria hao polisi wangalipaswa kuwakamata bila kuwadhalilisha na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria!!! Kumpiga mtu hata kama kakosa ni kosa kisheria! Huwezi kuilinda sheria kwa kuvunja sheria! Tafakari!!!
 
gud polis jamii, ningetamani waende UDOM ndo wangepata wangi xana wangetembeza viboko hadi wachoke.
 
Hii habari jan niliona katika gazeti moja la udaku lakini sikuisoma kwa makini hapa sasa nimeelewa kinachoendelewa

Kwa bahati mbaya, mimi siyaamini kabisa magazeti ya udaku. Kwa kuwa hutoa habari 'zilizoungwa' ile mbaya au hata za kutunga chini ya mwembe ili kupata soko.
 
Jaman sasa imekua ni kero, inamana kila mwanamke anayeonekana ucku akijuza ni mwanachuo? Mbona mnakuza mambo,inamana wanachuo ndo wana maisha magum kulko watu wote mpaka kufkia hatua ya kujuza. Tafakar!
 
Back
Top Bottom