DOKEZO Wanafunzi wa chuo kilichofungiwa Mwanza ‘walia’ ada zao kuzuiliwa

DOKEZO Wanafunzi wa chuo kilichofungiwa Mwanza ‘walia’ ada zao kuzuiliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
WANAFUNZI 33 wa udaktari wa binadamu waliohamishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kutoka Chuo Kikuu cha Mwanza (MzU) kwenda Chuo Kikuu cha Katoliki cha Sayansi na Afya Shirikishi (CUHAS), wameiomba serikali kuingilia kati ili kupatikana ada zao Sh. Milioni 73 zilizozuiwa na chuo hicho.

Wanafunzi hao ni kati ya 300 wa shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu walioondolewa MzU na kupelekwa CUHAS kwa ahadi ya ada zao kuhamishiwa wanakopelekwa, lakini imekuwa kinyume chake na kusababisha wazuiwe kuendelea na masomo na kufanya mitihani.

Waliondolewa chuoni hapo Disemba 2, 2025 baada ya TCU kukifungia MzU kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Udaktari wa Binadamu kwa mwaka wa masomo 2025/26, baada ya chuo hicho kubainika kudahili wanafunzi mara kumi zaidi ya idadi iliyoruhusiwa kisheria (60).

Hata hivyo, baada ya miezi takribani mitatu ya masomo baada ya uamuzi huo, wanafunzi hao wameanza kupata changamoto ikiwemo kuzuiwa na vyuo vilivyowapokea, kufanya mitihani na kuhudhuria masomo kutokana na ada zao kutohamishwa mpaka sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza Februari 25, 2026, Kiongozi wa wanafunzi 33 wa udaktari waliokumbwa na changamoto hiyo, Rachel Erick ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza shahada ya udaktari wa binadamu chuo cha CUHAS, amesema wamefuatilia ada zao kwa miezi mitatu sasa bila mafanikio.

“Tulihadiwa kwamba ada zetu zitahamishwa kwenye vyuo husika tunavyosoma, sisi wanafunzi 33 tunadai jumla ya Sh. Milioni 73 ambazo tulikuwa tumezilipa huko Mwanza University, na hizo ada tuliambiwa kwamba zitahamishwa kuja chuoni Bugando lakini tumefuatilia bila mafanikio yoyote,” amesema Rachel.

Ameongeza kuwa wamefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuandika barua tano, kufika ofisini mara nne, kuandika barua za mtu mmoja mmoja na kuzipeleka, pamoja na kuandika barua pepe lakini hazikuwahi kujibiwa.

“Tumejaribu kwa namna mbalimbali kufanya majadiliano nao ili tupate majibu kuhusu ada zetu lakini hakuna mafanikio na juhudi zetu zimegonga mwamba kwa sababu hawatupi majibu yanayoeleweka,” amesema Mwanafunzi huyo.

Kutokana na changamoto hiyo, ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Ofisi ya Rais – Tamisemi kuwazingatia na kuingilia kati suala hilo ili kupata ufumbuzi wa kudumu na waendelee na masomo yao bila kubughudiwa.

“Sisi ni madaktari wa kesho tunapaswa kuwa madarasani na kwenye vipindi vya masomo lakini tunaacha vipindi na masomo tunafuatilia ada ambazo tulitoa cash (fedha taslimu), lakini ada zetu imekuwa ni usumbufu hatulipwi ada zetu, tunaomba sana serikali mtuzingatie ada zetu zirejeshwe,” amesisitiza mwanafunzi huyo.

Naye, Enos Elias amebainisha kuwa kwa sasa wanapitia changamoto mbalimbali kutokana na sakata hilo ikiwemo kuzuiliwa kufanya mitihani na chuo cha CUHAS ambacho kimesisitiza kwamba hawawezi kufanya mitihani bila ada hizo kuwasilishwa.

“Ni miezi miwili sasa tunasoma huku Bugando tumekuwa kama tunasoma bure kwa sababu ada tulilipa kwingine lakini huku ada bado hazijawekwa, kwahiyo na wenyewe pia uvumilivu umefika mwisho wakatutaka tutafute ada, hivyo tumezuiliwa kufanya mitihani mpaka hatua ya mwisho tumeandika barua ya kuji-committ kwamba ndani ya wiki mbili hizo tutakuwa tumeshalipa ada,” ameeleza Elias.

Akitolea ufafanuzi wa kutoonekana ada hizo, Mshauri wa Chuo Kikuu cha Mwanza (MzU), Charles Budede ameeleza kuwa fedha hizo tayari chuo kilikuwa kimeshazitumia katika kulipa mishahara ya walimu, kuongeza walimu, kurekebisha miundombinu ya kujifunzia ikiwemo maabara, majengo na maktaba, kabla ya uamuzi wa serikali kukifungia na kuhamisha wanafunzi hao.

Amesisitiza kuwa chuo hakikuwa na dhambi kutumia fedha hizo kukidhi mahitaji mbalimbali na kutimiza matakwa yaliyotolewa na Serikali, huku akiitupia lawama TCU kwa kuleta sintofahamu na usumbufu huo kwa wanafunzi.

“Hata hivyo admission policy (sera ya udahili) iko wazi kwamba fedha inaweza kurudishwa katika mazingira gani, mfano kama mwanafunzi amepata ugonjwa ghafla na kushindwa kuendelea na masomo, au kama kuna kozi fulani ilikuwepo na inaendelea lakini sasa chuo kimeamua iondolewe hapo wanafunzi watarudishiwa fedha,” amesema Budede.

Ameongeza; “Lakini kwenye hili ni tofauti kwa sababu tunapaswa tujiulize nani alianzisha mchakato wa kuwaondoa hao wanafunzi? siyo sisi ni TCU wenyewe, kwa maana hata sisi ni wahanga wa hili jambo.”
 
Back
Top Bottom