Siwatetei ila sidhani kama wanafunzi wengi huwa tunafanya tafiti za kina
pale tunapotaka kujiunga na vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu
sidhani kama wengi huwa tunazingatia kufatilia usajili wa hivi vyuo na hata
usajili wa kozi mbalimbali sababu laiti kama tungekuwa tunaangalia hivi vitu
mapema hivi vyuo hakika visingekuwa miongoni mwa machaguo yetu kabisa
na hizi shida saiv zisingekuwepo hii nchi imeshavurugika umakini na jitihada
zako ndo unaweza kukufanya usipate taabu hili tatizo sio la kutatuliwa leo
kutokana na mazoea ya serikali yetu laiti hawa wanafunzi wangekuwa makini
hii shida isingekuwepo hili ni funzo kwa wanaojiandaa kuingia vyuoni mwaka huu
na walio shuleni wasome kwa bidii ili wasije chaguliwa vyuo visivyo kidhi mahitaji ya mitaala
na kozi wazipendazo kusoma katika Elimu ya juu
Mkuu nakubaliana na mawazo yako ila naomba nikurekebishe kidogo.
1. Mwanafunzi anapochagua chuo anapewa nafasi tano (5 Choices) za kuchagua chuo au kozi anazotaka kusoma
2. TCU haimpangii mwanafunzi chuo au kozi nje ya zile 5 selections za mwanafunzi alizojaza kwenye profile yake kupitia CAS
3. Kuna TRansfer pia - wanafunzi wengi walioko KIU waliingia pale baada ya kutemwa kwenye CAS sababu ya ushindani. baada ya nafasi kwenye vyuo vingi vya afya kujaa KIU ilikuwa ina nafasi nyingi tu kwenye mtandao wa TCU. wengi waliomba nafasi za afya KIU waliingia kwa mfumo huo.
4. Transfer za ndani - (internal Transfer) wanafunzi wengi wa KIU wapo walioomba kozi tofauti kabisa mfano BSc Computer Science na kisha kufanya internal transfer wao wenyewe chuoni kwa ridhaa yao na kukubaliwa na chuo.
5. TCU sidhani kama wanawachagulia watu programme au kozi za kusoma bila ridhaa yao.
6. Ushindani wa wanafunzi kwenye kada ya afya kwa mwaka 2014/15 ulikuwa mkubwa sana kiasi ambacho wengi waliiomba kada za afya waliishia kukosa kutokana na ushindani mkubwa.
baada ya huo ufafanuzi hapo juu naomba uelewe kuwa uchaguzi upo kwa mwanafunzi mwenye na kitu kikubwa ni ufaulu wake ndio utakao mpeleka kwenye chuo kizuri na kozi nzuri anayoitaka.
Tuepuke lawama kuwatupia TCU wakati sisi wenyewe wanafunzi ndio chanzo cha matatizo yote