Msafiri Kasian
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 2,133
- 661
- Thread starter
-
- #21
hivi bado vitoto sana na ni chini ya miaka 20 ..nadhani umri unawaruhusu kufanya haya...
nakumbuka enzi zangu niko pale Tboys nlikuaga naibuka disco vumbi night ni noma kila siku...
na ukikutana na mimi utaeza kufikiri nsapoteza mwelekeo ila mwisho wa siku nkatoka na DVSION ONE Huyoo nkasepa mlimani..
lo tukikutana huezi amini..ni umri tuu huwa unapita
hivi bado vitoto sana na ni chini ya miaka 20 ..nadhani umri unawaruhusu kufanya haya...
Nakumbuka enzi zangu niko pale tboys nlikuaga naibuka disco vumbi night ni noma kila siku...
Na ukikutana na mimi utaeza kufikiri nsapoteza mwelekeo ila mwisho wa siku nkatoka na dvsion one huyoo nkasepa mlimani..
Lo tukikutana huezi amini..ni umri tuu huwa unapita
mimi zaidi,jinsi walivyokuwa wakifuatilia hyo mistari ya nyimbo na kukata viuno! Nilitamani hata kuwauliza kama na kusoma ndo hivyohivyo.
Hongera sana Kasim Kasian! Hiyo ndio maana halisi ya taaluma ya Ualimu. Ualimu si kuwamezesha wanafunzi theory kisha wanafeli, bila kujua kwa nini? Kufanya hivyo ndiko kunakowatofautisha Waalimu na form Six leaver au wale wanaodandia fani au kufundisha uchochoroni. Tunapaswa kuhakikisha watoto wanalelewa katika misingi inayofaa. Kama kila Mwalimu akifanya kama wewe thamani ya Mwalimu itarudi. USIOGOPE!! UTAPATA FADHILA NYINGI, ACHANA NA WATU WANAKUVUNJA MOYO. Hata mimi nitakuunga mkono....
natumia nokia e5 kwenye jf sijui like unatupia vp we ni mzalendo wa kweli wa malezi ya kizazi kijaacho lkn ndipo tulipofikia ukitaka kuamini watoto wa leo 4m 4 hawaogopi, chukua namba ya simu mrushie elfu tano kwa tigo pesa halafu mwambie apande pikipiki aje guest fulani anakuja
Watoto wenyewe mnazalia wazazi wenu ninyi mnakimbilia mijini mnajifanya mnatafuta maisha.
Hivi babu na bibi "wazazi wako" wanaweza kuwa na mbio zakukimbizana na wajukuu? hasa hawa mnao walea huku mijini mkiona mambo magumu mnawahamishia vijijini kwa wazazi wenu.
Lazima tufike mahali tulee wanetu wazazi walitulea sisi tunapo kwepa majukumu yetu kwakupeleka watoto Vijijini walelewe na wazazi wetu "bibi na babu zao" matokeo yake ndo hayo wazee umri umekwenda muda wakufuatilia masomo yao hawana nikipindi chao chakula mafao.
Nashukuru mdau kwakuliona hilo ila ulipaswa kuwashauri ingawa siyo lazima wafuate utacho washauri ila ungekuwa umetimiza wajibu wako kama mzazi/mshauri angalao baadae waweze kujutia kutokushika ulilo washauri hapa Jf sidhani kama wanamuda wakuperuzi.
Wakifeli mitihani utawasikia "yakhe baraza la mitihani linatuonea sisi waumini wa dini ya kii*#@&".
Wakifeli mitihani utawasikia "yakhe baraza la mitihani linatuonea sisi waumini wa dini ya kii*#@&".
Hapo wakifeli lawama lukuki kwa walimu,tena wengine wanalaumu NECTA nakumbuka matokeo ya form 4,2010 kwa vile ulikua mwaka wa uchaguzi wakasema walimu waliosahihisha walikua CHADEMA nilicheka sana,yaani watu wanasingizia siasa kila sehemu.Leo niliingia SALUNI
moja amitaa ya Holili(BODA)-Moshi mida ya saa 11 jioni,kwaajili ya
kupunguza nywele.Nikawakuta wanafunzi wawili wa kike(kati ya kidato cha 2
hadi 4). Kinyozi naye amekaa kwa pembeni,anatafuna Mirungi na Big G
huku wakipiga stori.Matendo niliyoyaona ambayo siwezi kuyaandika,ni
kwamba binti mmoja kati ya wale alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na
kinyozi yule.Kinyozi akaanza kunihudumia huku akijisifu kuwa yeye
anafahamika sana,punde si punde wakaingia wanafunzi wengine wawili wa
kike.Hawa walikuwa ni wa form 4(mmoja alikuwa na kitabu cha chemistry
form 4) ktk shule moja hapa holili.Kinyozi akanifinya kidogo,akaniambia
"sinimekuambia nafahamika? Hawa wote nawanyoa mimi" akawasha
muziki,wanafunzi wakaanza kucheza hapo,mara nyingine anaacha
kuninyoa,anacheza nao kidogo.Ni mengi nimeyashuhudia jamani. Sasa
ikabidi,wale wasichana wamkazanie jamaa aninyoe haraka "wewe vipi? mnyoe
kaka wa watu haraka unamchelewesha!"
Sasa mimi nikajiuliza,hizi division 4 and 0 zitapungua kwa hali kama
hi? Na maambukizi ya magonjwa ya zinaa je?
MAONI YANGU: Wazazi wenye watoto wanaosoma shule za kutwa,muwe makini
na watoto wenu kwasababu,wengi wanaharibikia mitaani,disco na sehemu
kama hizi alafu mwisho wa siku wanafeli masomo yao,alafu lawama zote
anatupiwa mwalimu shuleni na serikali.