Leo niliingia SALUNI
moja amitaa ya Holili(BODA)-Moshi mida ya saa 11 jioni,kwaajili ya
kupunguza nywele.Nikawakuta wanafunzi wawili wa kike(kati ya kidato cha 2
hadi 4). Kinyozi naye amekaa kwa pembeni,anatafuna Mirungi na Big G
huku wakipiga stori.Matendo niliyoyaona ambayo siwezi kuyaandika,ni
kwamba binti mmoja kati ya wale alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na
kinyozi yule.Kinyozi akaanza kunihudumia huku akijisifu kuwa yeye
anafahamika sana,punde si punde wakaingia wanafunzi wengine wawili wa
kike.Hawa walikuwa ni wa form 4(mmoja alikuwa na kitabu cha chemistry
form 4) ktk shule moja hapa holili.Kinyozi akanifinya kidogo,akaniambia
"sinimekuambia nafahamika? Hawa wote nawanyoa mimi" akawasha
muziki,wanafunzi wakaanza kucheza hapo,mara nyingine anaacha
kuninyoa,anacheza nao kidogo.Ni mengi nimeyashuhudia jamani. Sasa
ikabidi,wale wasichana wamkazanie jamaa aninyoe haraka "wewe vipi? mnyoe
kaka wa watu haraka unamchelewesha!"
Sasa mimi nikajiuliza,hizi division 4 and 0 zitapungua kwa hali kama
hi? Na maambukizi ya magonjwa ya zinaa je?
MAONI YANGU: Wazazi wenye watoto wanaosoma shule za kutwa,muwe makini
na watoto wenu kwasababu,wengi wanaharibikia mitaani,disco na sehemu
kama hizi alafu mwisho wa siku wanafeli masomo yao,alafu lawama zote
anatupiwa mwalimu shuleni na serikali.