Adaiwa kutaka kumbaka mwenzao

Ni mwalimu wao wa nidhamu

Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Bulongwa kilichoko Wilaya ya Makete mkoani Iringa, wamemuua kwa kumshambulia kichwani mkufunzi wa chuo hicho, Dk. Jumbe Mafingo, kwa madai ya kupinga jaribio lake la kutaka kumbaka mwanafunzi mwenzao.

Taarifa za awali za makachero wa polisi zilieleza kuwa mkufunzi huyo aliuawa baada ya kutuhumiwa kwamba alitaka kumdhalilisha kijinsia mwanafunzi wa kike, Jean Laison Mwakabuta kwa kutaka kumbaka.

Tukio hilo la kuuawa kinyama kwa mkufunzi huyo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, lilitokea juzi usiku nyumbani kwake mjini hapa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, Dk. Mafingo alifikwa na umauti baada ya mwanafunzi huyo kuamua kwenda nyumbani kwake usiku ili kumkabidhi maelezo yake ya kimaandishi kuhusu sababu zilizomfanya alale nje ya chuo.

Ilielezwa kuwa muda mfupi baada ya kuingia kwenye nyumba ya mwalimu huyo, mwanafunzi huyo alianza kupiga kelele kuwa anabakwa.

Alisema kufuatia kelele hizo, wanachuo wengine waliamka katika vyumba vyao na kwenda hadi eneo la tukio na kuanza kumshambulia kichwani mkufunzi huyo hadi kumuua.

Kamanda Mangalla alisema Dk. Mafingo aliuawa kwa kushambuliwa na kitu kizito kichwani.

Huyu Jean Laison Mwakabuta, aliambiwa na Dk. Mafingo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, aandike maelezo ya maandishi kwa sababu gani alilala nje ya chuo,...baada ya kuandika maelezo hayo, aliamua kuyapeleka nyumbani kwa mkufunzi huyo usiku, sasa baada ya kugonga mlango na hatimaye akaruhusiwa kuingia, alianza kupiga kelele kwamba anabakwa
na ndipo wanafunzi wenzake waliposikia kelele wakaamka na kukimbilia eneo hilo na kumshambulia mkufunzi huyo hadi kufa, alisema Kamanda Mangalla.

Ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, uongozi wa chuo hicho cha Bulongwa ulitoa ridhaa kwa wanachuo wote kwenda kutembea nje ya chuo kwa lengo la kuwapunguzia msongo wa mawazo ya masomo na Jean Laison Mwakabuta hakurejea chuoni hadi siku iliyofuata.

Kamanda Mangalla, alisema wanachuo wanne akiwamo mwanafunzi Jean, wametiwa mbaroni kuhusiana na mauaji hayo.

CHANZO: NIPASHE

maoni: hivi watu wanashindwa kuoa wake zao wa halali, naona kina dada nao wameshituka sasa