Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

duh, kumbe viko vingi? kuna haja ya katiba mpya...........
mkuu hta chuo kikuu cha sayansi na technolojia mbeya(MUST),kuna wanafunzi walisimamishwa kufanya chuo kisa hawakufanya mtihani siku ya sabato
 
asante, huenda kama wamo humu utawasaidia sana.........
 
Join Date : 23rd July 2013
Posts : 1
Rep Power : 0
Likes Received 0
Likes Given 0

Gureni naona mjadala huu umekuvutia ufungue anuani JF
 
kumbuka wamekosa haki katika nchi yao....
 
wazushi tu hao, mtihani ndiyo maisha kwani ni anasa hiyo , unafanya na hapo hapo kwenye mtihani huku unamuabudu akupaishe u score vizuri, sababu hapo ulipo ni wewe na paper na mungu wako
 
you will have me excused this time, badala ya watu kutoa hoja kama kufukuzwa kwao ni halali kisheria wameanza kuelezea hisia na logic, ila nafikiri tuliongea kama engineeers au madokta, na nina wasi wasi kama kulikuwa na mwanasheria yoyote.
 
X-MASS ni sikukuu ya WAPAGANI. mimi ni mlutheri but najua hii sikuku ni ya MAGUMASHI ya wazungu wapagani. KWANZA YESU HAKUTAKA KABISA TUKUMBUKE SIKU YAKE YA KUZALIWA,. ALITAKA TUKUMBUKE PASAKA TU. NA YESU ALIZALIWA KIPINDI CHA BARIDI UYAHUDINI SIO KIPINDI CHA BARIDI ULAYA.....ILA KWA WASABATO MIMI HUWAITAGA NUSU WAYAHUDI COZ WAMEBEBA MENGI KUTOKA HUKO, THOUGH NAKUBALIANA NAO KUWA SIKU YA SABATO NI JUMAMOSI . TATIZO LA WASABATO NI HILI" WANAJIONA WAO NDIO WAKRISTO WALIO BORA ZAIDI YA WENGINE, YANI KAMA VILE WAO NDIO WANA V.I.P TIKETI YA KWENDA MBINGUNI" NA SIE WENGINE HATUNA. HAWATAKI WAOANE NA WAKRISTO WENGINE, YANI WAO KWA WAO WENYEWE
 
Tatizo jingine la wasabato wote niliokutana nao kutoka skul mpk hapa, ni kuwa wamejichagulia dhambi za kufanya na nyingine ndio wanaiona dhambi zaidi. Yani siku zote nyingine ni mastarehe, bata na madhambi yote unayoyajua wewe eti ikifika jmosi, ndio watakatifu, mi hii naona ni kumtania na kumkashifu mungu, kama jamaa mmoja alivyosema kuwa wanaishi na mademu but hawataki kufanya pepa jmosi....huko si kumdhihaki mungu, lakini ni wabishi balaa!!! But mimi kwangu nina madhambi yangu but naamini kila siku ni ya mungu. Iwe j3 au j2. Mkumbuke mungu kila siku..." kesheni mkiomba" mkumbuke muumba wako siku za ujana wako" sio kila jumamosi.
 
SI WAENDE VYUO VYA JMT? Kile chuo ni cha Moravian. Walipaswa kuangalia MoU baina ya serikali na Wamoravian kabla ya kujiunga.Uhuru wa kuabudu uko serikalini na sio kwenye vyuo binafsi.

Historia iko wazi kuwa Sabato ya Biblia ni Jumamosi. Ndio maana Wakristo wote wanatambua Ijumaa Kuu kama siku aliyokufa Yesu, Akalala kaburini Jumamosi na Kufufuka Jumapili. Hivyo, Sabato ya Kweli ni Jumamosi, hapo hakuna ubishi. Wote wanaosali Jumapili wanajua wazi kuwa ni siku ya kuabudu jua (sun-day) ambayo ilikuwa ni ibada ya mizimu zama zile. Kuhusu wale wapendwa kufukuzwa kwa sababu ya kugoma kufanya mtihani siku ya Jumamosi, wako sahihi kabisa. Imani yao inawataka wasifanye kazi yoyote siku ya Sabato (Angalia Kutoka 20:8-11). Hivyo, waliowafukuza wamevunja Katiba ya nchi. Ingekuwa mimi, ningewaburuza kotini hadi wangefunga hicho chuo kwa fidia kubwa watakayotakiwa kunilipa.

Hivi karibuni Waislamu walipiga kelele kuwa waachiwe kuchinja, kwani hiyo ni ibada kwao. Wengi humu JF mlitetea sana hoja hiyo, mbona hawa jamaa Wa Sabato mnashindwa kuwatendea haki? kwao kupumzika siku ya Jumamosi ni Ibada na utii kwa Mungu wao. Wapewe haki yao.
 
Sijakataa uhuru wa kuabudu. Ninachosema ni kuwa Wamoravian kwa imani yao haitambui Jumamosi kama ni siku ya mapumziko. Chuo ni chao, kwa ajili ya manufaa yao na hasa kukuza imani yao. Mtu yeyote anayekwenda pale anapaswa kukubaliana na mipango yao yote. Kama anaona kwake yeye ni kikwazo anapaswa kutafuta chuo mahali pengine patapokubaliana na imani yake. Ukienda chuo kikuu cha kiislam cha Morogoro kwa mfano, ukaenda na kitimoto yako bwaloni, halafu useme nina uhuru wa kuabudu, sidhani kama utakubalika
 
ni kweli, so tunawasaidiaje?
 
Mkuu hebu angalia hapo kwenye RED utafakari tena ulichokiandika..........
 
TEKU waliamua kufuata mkondo wa chuo cha kitaifa hivyo inabidi wawavumilie wenye imani tofauti. La sivyo watamke wao ni chuo kikuu cha wamoravian nasi hatutakiuwa na lingine bali kuwaachia chuo.

Mdogo wangu, imani ni kwa ajili ya ustawi wako. Mungu ni mwenye huruma na wala hawezi kukuhukumu kwa jambo husilo na uwezo nalo. Mungu amekupa utashi kung'amua mema na mabaya hivyo kuacha kufanya mtihani siku ya Jumamosi ni kujifanya punguani.

Mbona dhambi nyingi tu tunatenda kinyume na usabato na tunaomba msamaha kwa muumba? Kama kufanya jambo jema kama mtihani siku ya Sabato ni kosa, basi acha hilo kosa liwe juu ya Chuo sio wewe.

Vinginevyo utafukuzwa chuo, na Mungu hatakusamehe kwa hilo kwani amekupa akili na utashi.

Ningejua huja baadae! Nilisoma chuo, UDSM na rafiki yangu kipenzi msabato kama wewe. Alitaka kuhairisha mojawapo ya mtihani uliokuwa umepangwa siku ya Jumamosi ili afanye na watu wa Supplementary mwezi wa tisa. Hii ilikuwa mwaka wetu wa mwisho, nikamuuliza itakuwa vipi asipofaulu huo mtihani mwezi wa tisa, inamaana alitakiwa ku-carry somo mwaka unaofuata kitu ambacho kama kingetokea ina maana angetakiwa kumaliza chuo mwaka mwingine. Swali lingine likaja, vipi ikitokea mtihani ukapangwa tena Jumamosi? Baada ya kumuelezea hizi hatari, akasema Mungu anisamehe, akafanya mtihani.

Ijulikane kwamba vyuo vinakuwa na upungufu wa kumbi kwa ajili ya mitihani kwa wanafunzi wengi kwa kipindi kifupi hivyo suala la kufanya mitihani Jumamosi na pengine Jumapili haliepukiki. Mimi binafsi wakati nasoma UDSM niliwahi kufanya mitihani na majaribio siku ya Jumapili. La muhimu kama msomi unaangalia ratiba yako, kama mtihani ni 4 asubuhi, basi unaenda misa ya asubuhi sana kabla ya mtihani. Hili suala nimelishuhudia hata Uingereza, mitihani vyuoni inafanyika mpaka Jumamosi na huko kuna wasabato pia.

Kuna majuto mengi kwa watu waliokariri biblia na kujiondoa ufahamu. Pole yao, Roho Mtakatifu akiwashukia watajua mahali walipokosea.
 
Nadhani ninamaanisha nilicho kiandika, lakini kama una tafakuri tofauti na nilichokisema unaweza kusema pengini itasaidia kunitoa katika uewelewa huo. Pia wamoravian wenyewe wana nafasi kubwa kunisahihisha ikiwa nitakuwa nimewaelewa tofauti na nilivyoeleza mwanzo. Asante kwa kusoma mchango wangu
Mkuu hebu angalia hapo kwenye RED utafakari tena ulichokiandika..........
 
Ukijijua wewe ni mwanafunzi wa chuo zingatia yafuatayo
1. Nidhamu
2. Academics
3. Socialization
ibada ifanye ni tabia ya kila siku kwa mungu bila unafki, hatojali umemwabudu jtatu,ama jmosi yeye atajibu tu.mungu hutaka ibada ya kweli na sio siku ya kweli ya kufanya ibada.b brave men...na ma dr. Hawa wakijua tu mnawachokoa ndo wanaweka kikwazo ambacho hata ukajipige kwenye jiwe hupiti so utanufaika nini na kizazchako kwa kuitetea sabato na kuipuuza alimu yako kwa amblela ya ibada?
 
Nani kasema sabato ipo hadi leo? soma wakolosai 2:16-17 sabato ilifutwa mwaka 33 AD
 
Tusichanganye Maisha ya Chuo kikuu na Misimamo ya kiimani ambayo kamwe haiboreshi mahusiano yetu na MUNGU.Mimi nilipokuwa UDSM niliwahi kwenda kufanya Test Jumapili baada ya Ibada na HILI halikuharibu kabisa UHUSIANO WANGU NA MUNGU.Anyway, kama misimamo kama hii ingewaongezea wahusika neema ya kushinda dhambi, kuwa waaminifu kazini, kuwapenda wengine nk alau ningeona hao wanachuo wana hoja.
 
Imani ni ngumu sana maana kuna jamaa yangu kipindi cha sensa aliacha kwa sababu kilikua kinaenda hadi jmosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…