Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ingawa mjadala huu ni wa muda mrefu kidogo, ila mwanzoni mwa mwezi huu, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilitoa hukumu ambayo inawapa haki wanafunzi kama hawa kuweza kusoma bila haki zao za kuabudu kuingiliwa na serikali au mamlaka zingine. Haki za Binadamu wananchi wa Tanzania wanazohakikishiwa kwenye katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Haki zingine za kimataifa ambazo Tanzania imeridhia kuzikubali, inakataza kuwepo kwa sheria nyingine zozote ambazo zinakinzana na kuzuia raia wa Tanzania kutokuwa huru na kufurahia haki zao za msingi za binadamu ikiwemo ya kutokuzuiwa kupata elimu kwa sababu ya misingi ya dini zao.
Katika mjadala huu ambao umeendelea kwa muda mrefu hapa jukwaani, wengi wametoa maoni tofauti tofauti wakishuku au kupinga haki ya wanafunzi hawa kuendelea na dini na imani zao hasa katika vyuo hivi binafsi ambavyo vina sheria zao ambazo walikubaliana nazo wakati wanaomba kujiunga. Tafadhali soma nakala ya HUKUMU ya Mahakama ya Rufaa maana inaweza kusaidia kupanua upeo wetu wa kuelewa haki wanazopewa wananchi, hasa inapokuja kwa maswala ya uhuru wa dini.
Wengine wametoa changamoto ya maisha binafsi ya wanafunzi hao ambayo huenda yanakinzana na madai yao ya kidini. Ingawa mimi binafsi nakubaliana asilimia 100 na changamoto hii maana kama unadai kuonewa kidini, angalau elekeza maisha yako kikamilifu kwa kufuata maadili ya dini hiyo. Lakini inaposoma hukumu hii, unagundua kwamba "Dini" au "Imani za Kidini" kisheria inapewa tafsiri pana kabisa na tafsiri binafsi za kidini nazo zina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo mbele ya sheria, kinachotakiwa tu ni kwamba ile haki inayodaiwa inadaiwa kwa dhati, katika kipengele tu cha haki hiyo na kwamba dhamiri ya mhanga wa kunyimwa haki hiyo anaamini kwa dhati kabisa kwamba (kwa tafsiri hii), kufanya mtihani siku ya Jumamosi hakuridhiwi na maadili ya imani yake. Kwa hiyo utaona swala la dhamira binafsi ni muhimu katika sheria, na ingawa ni kinyume kabisa kimaadili, lakini mbele ya sheria, wanafunzi hawa bado wana haki ya kikatiba na kisheria kutokufanya mitihani siku ya Jumamosi na kuruhusiwa kuendelea kusoma (labda kwa kufanya mitihani siku nyingine ya wiki) kama dhamiri yao inawahimiza kufanya hivyo hata kama kwenye maeneo mengine ya kidini (mfano kingono kama ilivyoelezwa awali), wanaweza wasiwe makini sana, lakini kinachohesabiwa ni Dhamiri binafsi ya mhusika.
Niwatakie siku njema na wiki njema.
nauliza tu,hivi wasabato wanaosoma nje ya nchi katika nchi zisizo na mifungamano ya dini hizi kuu mbili tulizonazo hapa nchini(mf.china, urusi n.k), huwa nao wanagomea mitihani???duuuh....kuna nchi siku za chrismass na eid ni darasani kama kawaida. kwa upande wa Tz mlimani nimeshashuhudia watu wanafanya test siku za chrismass na eid na mhadhiri anakwambia "huo ndio muda pekee ambao niko free" , kwa hyo una hiari uende kwenye test au ubaki na imani yako ya kusherehekea eid au chrismass.....mhh mambo ya imani kaazi kweli kweli!!!
SI WAENDE VYUO VYA JMT? Kile chuo ni cha Moravian. Walipaswa kuangalia MoU baina ya serikali na Wamoravian kabla ya kujiunga.Uhuru wa kuabudu uko serikalini na sio kwenye vyuo binafsi.
Historia iko wazi kuwa Sabato ya Biblia ni Jumamosi. Ndio maana Wakristo wote wanatambua Ijumaa Kuu kama siku aliyokufa Yesu, Akalala kaburini Jumamosi na Kufufuka Jumapili. Hivyo, Sabato ya Kweli ni Jumamosi, hapo hakuna ubishi. Wote wanaosali Jumapili wanajua wazi kuwa ni siku ya kuabudu jua (sun-day) ambayo ilikuwa ni ibada ya mizimu zama zile. Kuhusu wale wapendwa kufukuzwa kwa sababu ya kugoma kufanya mtihani siku ya Jumamosi, wako sahihi kabisa. Imani yao inawataka wasifanye kazi yoyote siku ya Sabato (Angalia Kutoka 20:8-11). Hivyo, waliowafukuza wamevunja Katiba ya nchi. Ingekuwa mimi, ningewaburuza kotini hadi wangefunga hicho chuo kwa fidia kubwa watakayotakiwa kunilipa.
Hivi karibuni Waislamu walipiga kelele kuwa waachiwe kuchinja, kwani hiyo ni ibada kwao. Wengi humu JF mlitetea sana hoja hiyo, mbona hawa jamaa Wa Sabato mnashindwa kuwatendea haki? kwao kupumzika siku ya Jumamosi ni Ibada na utii kwa Mungu wao. Wapewe haki yao.
Historia iko wazi kuwa Sabato ya Biblia ni Jumamosi. Ndio maana Wakristo wote wanatambua Ijumaa Kuu kama siku aliyokufa Yesu, Akalala kaburini Jumamosi na Kufufuka Jumapili. Hivyo, Sabato ya Kweli ni Jumamosi, hapo hakuna ubishi. Wote wanaosali Jumapili wanajua wazi kuwa ni siku ya kuabudu jua (sun-day) ambayo ilikuwa ni ibada ya mizimu zama zile. Kuhusu wale wapendwa kufukuzwa kwa sababu ya kugoma kufanya mtihani siku ya Jumamosi, wako sahihi kabisa. Imani yao inawataka wasifanye kazi yoyote siku ya Sabato (Angalia Kutoka 20:8-11). Hivyo, waliowafukuza wamevunja Katiba ya nchi. Ingekuwa mimi, ningewaburuza kotini hadi wangefunga hicho chuo kwa fidia kubwa watakayotakiwa kunilipa.
Hivi karibuni Waislamu walipiga kelele kuwa waachiwe kuchinja, kwani hiyo ni ibada kwao. Wengi humu JF mlitetea sana hoja hiyo, mbona hawa jamaa Wa Sabato mnashindwa kuwatendea haki? kwao kupumzika siku ya Jumamosi ni Ibada na utii kwa Mungu wao. Wapewe haki yao.
Sijakataa uhuru wa kuabudu. Ninachosema ni kuwa Wamoravian kwa imani yao haitambui Jumamosi kama ni siku ya mapumziko. Chuo ni chao, kwa ajili ya manufaa yao na hasa kukuza imani yao. Mtu yeyote anayekwenda pale anapaswa kukubaliana na mipango yao yote. Kama anaona kwake yeye ni kikwazo anapaswa kutafuta chuo mahali pengine patapokubaliana na imani yake. Ukienda chuo kikuu cha kiislam cha Morogoro kwa mfano, ukaenda na kitimoto yako bwaloni, halafu useme nina uhuru wa kuabudu, sidhani kama utakubalika
TEKU waliamua kufuata mkondo wa chuo cha kitaifa hivyo inabidi wawavumilie wenye imani tofauti. La sivyo watamke wao ni chuo kikuu cha wamoravian nasi hatutakiuwa na lingine bali kuwaachia chuo.
Mkuu hebu angalia hapo kwenye RED utafakari tena ulichokiandika..........
Nikirejea Ibara ya 19 ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977 inatoia Uhuru wa Mtu Kuabudu.......
Hali kwa Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji ni Tofauti kwani wanafunzi wapatao 8 wamefukuzwa Chuoni hapo kwa madai ya kutofanya mitihani iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Sabato kwamba kwa kanuni za Chuo hicho hiyo si sababu ya kumfanya mwanafunzi asifanye mitihani
Wanafunzi hao wapo mitaani kwa sasa wakisaka msaada wa kisheria
- Je yamkini wakati wanafunzi hao wanapokelewa hilo halikuwekwa bayana?
- Mbona Mitihani isiwe Jumapili?
- Wapi Uhuru wa Kuabudu kwa mujibu wa Katiba JMT na sheria?
Je mnawashauri nini wanajamvi?