Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Ni wapuuzi tu. Hayo ndio matokeo ya imani kali ya dini, wakiambiwa wajilipue watakwenda mbinguni hakika watajilipua. Wale wakristo tumeambiwa 'mpeni kaisari yaliyokua ya kaisari na mpeni mungu yaliyokua ya mungu' lakini mtu anataka kumpa mungu ya kaisari.
 
siyo kazi ya chuo kujuwa wewe ni sabato, mkristo. muislam, mpagani au la wewe unatakiwa kufuata sheria na taratibu unazozikuta pale, na unapokuwa unaaply chuoni jaribuni kusoma taratibu na mjitahidi hata kuwaulizia wenzenu walio watangulia kujuwa utaratibu wa chuo husika, siyo kuanza kuleta masuala ya ikitadi vyuoni, leo sabato, kesho masjid, keshokutwa kanisani,n.k sasa shule itapatikana kweli, sasa kama unaona huwezi kufanyakazi jumamosi unasoma ili iweje? ukiitwa kazini jumamosi kwamba kuna dharula inamaana hutaenda kuhudumia jamii, achene ujinga nyie someni kwanza
 

Kama kweli wao ni wacha mungu kama wanavyodai kwa nini wasiende kusomea uinjilisti kwenye vyuo vya kisabato ili wahubiri injili?Hii inanikumbusha jamaa mmoja msabato aliajiriwa mgodini kama accountant akaleta usabato wake kazini yeye siku ya jmosi haendi kazini ila anashinda anafukuzia loose-balls! Kwa kama miezi 3 walimvumilia kwa vile mkuu wake alikuwa mbongo then akaja mkuu mpya ambaye alikuwa mu-Austaralia: Mzungu alimuuliza what the HELL IS SDA? Na akamwambia achague either kazi au SDA!! Jamaa akawa mpole!
 
walipokuwa waapply hicho chuo hawakujua rules?kitendo cha wao kujiunga na TEKU maana yake TERMS AND CONDITIONS APPLY.waache mambo yao.Hiyo Udsm ipi unayosemea wewe?sie faculty of law tuliwahi kufanya test sikukuu na hakuna aliyebisha.sasa waendelee kukomaa lakini mwisho wa siku wao ndio wahanga.AKILI NYINGI NGUVU KIDOOOOGO!!
 

Hakuna mahali utakuta uhuru wa ain hiyo, ati kila kundi liwe na siku yake ya kuabudu na serikali i accomodate. Vipi sisi wa dini za asili, siku zetu za kwenda kutambika tusiende kazini pia?
 
TEKU waliamua kufuata mkondo wa chuo cha kitaifa hivyo inabidi wawavumilie wenye imani tofauti. La sivyo watamke wao ni chuo kikuu cha wamoravian nasi hatutakiuwa na lingine bali kuwaachia chuo.
Chuo cha Kitaifa kinakuwaje kwenye hili?
 

........
Hawa wanaleta ushamba na dini...
 

Umenena vema.
 

Biblia inasema Hakuna mwanadamu anayehasabiwa haki kwa Matendo ya Sheria.
 

Ameeen.
 

Kwakweli kati ya vitu vinavyoturudisha Nyuma na kuwa Pazia machoni mwetu ili Mabepari waendelee kuchota Malighafi zetu ni DINI. NAJUA WAPO WATAKAO PINGA SANA LAKINI UKWELI NDO HUO.
 

Biblia inasema 'Amelaaniwa kila aliye chini ya Sheria na asiitimilize yote'. R/Mtakatifu hakai ktk mwili wenye laana. Leo hii tunashuhudia wazinzi wengi sana, mbona sijasikia wakiwapiga mawe ilihali Sheria inasema apigwe mawe mpaka afe!?
 
Ao hawajui kua hata vtab vyao vinawa asa wamshike sana elim
 
Wanataka kuweka sheria za kanisa chuo?! Si wakasomee kwenye vyuo vya uchungaji?!

Watu wa hivi wananiudhi sana, unakuta kwenye mambo mengine yote anafanya kinyume ila likija suala la siku ya sabato na mtihani basi hapo ndipo anaposimamia sabato!

Nataman kila mmoja angejua kuwa hizo ni siku tu, wala hazina uhusiano wowote na utakatifu! Jitahidi Kuwa na matendo mema, mengine yaliyobaki ni kwa neema tu ya Mungu wala sio kwa nguvu zetu!
 
Biblia inasema Hakuna mwanadamu anayehasabiwa haki kwa Matendo ya Sheria.

ni sahihi, yakupasa uwe na iman pia. Ukivichanganya vyote kwa pamoja, unapata haki kote kote. Wasabato wanaongozwa na sheria ya MUSA ambayo haiwez kuwakamilisha mbele za MUNGU. Wabadilike au waanzishe vyuo vyao
 
Aleyn na huku tena Upo? Natumain sasa hauna ubishi juu ya Sabato! Hiyo Wagalatia yote unayo ishikiria hakuna ata sehemu moja inayopinga sheria na vitabu vote vya Paul hakuna ata sehemu akipinga sheria! Ni wewe tu unavolitafsri neno vibaya.
Naomba utafute kitabu kiitwach, A day to remember kimeandikwa na George E Vandeman! Ata kwenye Internet kutafute. Hayo mambo unayapinga hapa utapata majibu! Agano, sheria, haki, mitume. Na mengine yote utapata hapo juu ya Sabato!
Narudia tena Aleyn soma hicho kitabu na wengine wote wanayoipinga au kutaka kujua Sabato!
 
Biblia inasema 'Amelaaniwa kila aliye chini ya Sheria na asiitimilize yote'. R/Mtakatifu hakai ktk mwili wenye laana. Leo hii tunashuhudia wazinzi wengi sana, mbona sijasikia wakiwapiga mawe ilihali Sheria inasema apigwe mawe mpaka afe!?

Naomba utafute kitabu kiitwacho When God made rest by George E Vandeman na kingine kiitwacho A day to remember By George E Vandeman! Vitakusaidia katika Haya yote!
 
Nani kasema sabato ipo hadi leo? soma wakolosai 2:16-17 sabato ilifutwa mwaka 33 AD

Wakolosai hiyo haisemi kua Sabato imefutwa huo ni uongo wa wazi kupotosha watu ni sawa na ule wa kusema Yesu alivunja Sabato kitu ambacho Si kweli!
Therefore let no one judge you in food or in drink, or regarding a festival or new moon or sabbaths.
Which are a shadow of things to come but the substance is of Christ. Colossians2:16-17
Haya Sabato imefutwa wapi sasa hapo?
 

.......................................................................................................................................


Asante sana Maswala kwa mchango wako mzuri...nami nina ya kuongea kidogo kuhusu hili...

Ndugu zangu kwanza tuelewe kile ni chuo cha BINAFSI na sio cha serikali....hivyo basi kina taratibu zake na kanuni zake na sheria zake. Hii ina maana yeyote anayejiunga na chuo ambacho ni binafsi shurti akubaliane na kanuni, taratibu na sheria za mahali hapo...HAIWEZWKANI UENDE MAHALI SIO KWAKO HALAFU UANZISHE SHERIA ZAKO....HAIWEZEKANI.. Haina tofauti na wanafunzi wa kiislamu wanaoenda kusomea udaktari wa mifugo (akiwemo nguruwe) halafu wanagoma kumtibu au kumshika nguruwe kisa ni "haramu" kwa imani yao...HUU NI UJINGA.

Haiwezekani wewe mkristo uende ukasome au umpeleke mwanao shule za kiislamu halafu mwanao aache kuvaa hijabu...maana hizo ndizo taratibu zao...Haiwezekani wewe muislamu uende ukasome au umpeleke mwanao akasome ktk shule za seminary za kikristo aache kwenda kanisani jumapili au kuingia vipindi vya maombi kila alfajiri...NASEMA HAIWEZEKANI.

Tukianza ku-entertain haya mambo ina maanisha... kama ni mashuleni au vyuoni basi masomo yafundishwe jumatatu hadi alhamisi tu na mitihani itungwe ndani ya siku hizo tu maana Ijumaa-Waislamu, Jumamosi-Wasabato na Jumapili-RC/Protestants...Hii kitu HAIWEZEKANI. Pia hatutaishia vyuoni...tutasogea hadi makazini...na kwenye semina n.k n.k n.k...NASEMA HAIWEZEKANI.

Umekuja kunitembelea kwangu au umekuja kukaa kwangu NI LAZIMA NA SIO OMBI (LABDA MIMI NDIO NIONE HURUMA) UFUATE TARATIBU ZA NYUMBA YANGU... Sio umekuja leo kesho utarudi usiku wa manane...ukitegemea tutakufungulia mlango...kwako hapa? Vivyohivyo na hili la wasabato...kama wameona kile chuo hakitendi haki waende ktk vyuo vyao (Vya kisabato) alaa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…