Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Nikirejea Ibara ya 19 ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977 inatoia Uhuru wa Mtu Kuabudu.

Hali kwa Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji ni Tofauti kwani wanafunzi wapatao 8 wamefukuzwa Chuoni hapo kwa madai ya kutofanya mitihani iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Sabato kwamba kwa kanuni za Chuo hicho hiyo si sababu ya kumfanya mwanafunzi asifanye mitihani

Wanafunzi hao wapo mitaani kwa sasa wakisaka msaada wa kisheria
  1. Je yamkini wakati wanafunzi hao wanapokelewa hilo halikuwekwa bayana?
  2. Mbona Mitihani isiwe Jumapili?
  3. Wapi Uhuru wa Kuabudu kwa mujibu wa Katiba JMT na sheria?

Je, mnawashauri nini wanajamvi?
 
Kwanza kabla ya mjadala kuendelea, ningependa kujua ni vitu gani ambavyo si ruhusa kwa SABATOS kuvifanya siku ya jumamosi, tukisha jua hilo then, tutaweza kuuweka mtihani katika kundi gani, baadae kutoa maamuzi, karibu..
 
Ya kaisari apewe kaisari na ya Mungu apewe Mungu, waache kuchanganya dini na taaluma, vyuoni si mahala pa kudumu ni sehemu za kupita tu na kila sehemu kuna taratibu zake, kila mtu kila sehemu akisema afanye kwa jinsi anavyoamini unadhani kuna la maana litaendelea kweli?
 
ni siku yao ya kuabudu.labda kuanzia jioni ya 12 ndio mtihani unaweza fanyika. hiyo ilikuwa kawaida katika UDSM chuo kongwe jumamosi test na mitihani ni usiku au jion kabisa.TEKU wanatapatapa watawarudisha hao
 
Nadhani wanafunzi waache ujinga, mtihani siku ya J1 wala J2 au siku zingine haina shida. Mbona Waislam wanafanya kazi Ijumaa? Mbona shuguli za chaguzi hufanyika J2?

Sabato ya kweli ni pumziko moyoni, lipatikanalo ndani ya Yesu pekee ambaye ni Bwana wa sabato. Siku zote ni za Mungu, hakuna hata moja ambayo ni ya shetani, na siku zote inabidi tumwabudu Muumba.

Kakika nchi za kiarabu, wakristo hukusanyika siku ya Ijumaa (J1 na J2) ni siku za kazi.

Alafu wakati leo hapa ni J1 kwingine ni Ijuma au J2. So kasome maandiko vizuri, wahsauri wanafunzi wenu wakafanye mitihani siku yoyote itakapotolewa.

Pia Yesu alisema msingi wa sabato ni kufanya mema, kama vile "kumokoa punda shimoni", mtijani wako na wa thamani sana kuliko thamani ya Punda!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kuna jamaa yangu ni msabato na anaishi na demu wake geto moja.linapofika swala la kufanya mitihani au presentation jumamosi alikua anagombana sana na ma doctor.siku moja nikamwambia mbona unaishi na mwanamke na mnazini huoni hiyo ni dhambi au dhambi ni kufanya kazi jumamosi?

Amenichukia mpaka leo.wakati mwingine haya mambo ya imani tunajichanganya sana.
 
TEKU waliamua kufuata mkondo wa chuo cha kitaifa hivyo inabidi wawavumilie wenye imani tofauti. La sivyo watamke wao ni chuo kikuu cha wamoravian nasi hatutakiuwa na lingine bali kuwaachia chuo.
 
wapumbavu hao wao walipokuwa wanafanya aplication TEKU hawakujua ni chuo cha dhehebu gan kwann wasingeenda kweny chuo chao arusha university ambacho kinatukuza sabato,kwanz din na elim ni tofaut j'mos ni siku ya kaz na siyo ya kuabudu!
 
wapumbavu hao wao walipokuwa wanafanya aplication TEKU hawakujua ni chuo cha dhehebu gan kwann wasingeenda kweny chuo chao arusha university ambacho kinatukuza sabato,kwanz din na elim ni tofaut j'mos ni siku ya kaz na siyo ya kuabudu!
Huenda pia kujiuliza kwamba wakati Chuo kinawaandikisha hakikujua kwamba kuna Wasabato?
 
TEKU waliamua kufuata mkondo wa chuo cha kitaifa hivyo inabidi wawavumilie wenye imani tofauti. La sivyo watamke wao ni chuo kikuu cha wamoravian nasi hatutakiuwa na lingine bali kuwaachia chuo.
Huenda lengo lao la awali la kupata idadi kubwa ya wanafunzi regardless ya imani zao lilitimia sasa wameamua kuwatimua waliozidi
 
SI WAENDE VYUO VYA JMT? Kile chuo ni cha Moravian. Walipaswa kuangalia MoU baina ya serikali na Wamoravian kabla ya kujiunga.Uhuru wa kuabudu uko serikalini na sio kwenye vyuo binafsi.
 
Walisoma By Laws za chuo wakati wa kujiunga au kurudisha form za kujoin na chuo? Wao kwa nini hawakuchagua vyuo vya kisababto kama wanapenda usabato? Chezea warumi weweee utageuka kuwa six leaver hata mahakama ifikie wapi!!

SAUT Mwanza walileta hizo nyodo, wakafukuzwa bila kurudishiwa chao. Wachache wakaomba msamaha wakasamehewa.

Afu wengi wa wanafunzi (Wasabato ) walio goma walikuwa wanaishi kama mke na mme bila ndoa, hivyo kukutanisha vikojoleo kwao ilikuwa kama kawa licha ya amri za Mungu kukataza. Tena kipindi hicho jmosi haikuwa siku ya masomo ila mwl aliweza kuomba wanafunzi kusoma siku hiyo. Tangia wasabato walete kimbelembele hadi leo jmosi ikawekwa kwenye time table kama siku ya j3 hadi Ijumamosi mapindi kama dawa na paper kama kawa J3 hadi Jmosi.

Bwana Yesu Asiwe.
 
TEKU waliamua kufuata mkondo wa chuo cha kitaifa hivyo inabidi wawavumilie wenye imani tofauti. La sivyo watamke wao ni chuo kikuu cha wamoravian nasi hatutakiuwa na lingine bali kuwaachia chuo.

Na ukiacha chuo unamkomoa nani?
 
Back
Top Bottom