Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Wanafunzi wa Kisabato Wafukuzwa TEKU kwa Kukataa Kufanya Mitihani Siku ya Sabato naomba muongozo wa kisheria

Hao nao waache upimbi wa kujifanya kuwa wao ni wayahudi kuliko wayahudi wenyewe, Mbona waislamu wanapiga pepa hadi Ijumaa? Mbona hapo SUA wakristo wanapiga pepa hadi J2 lakin hatusikii upunguani wowote kama huu?
 
Njia ile ni nyembamba iendayo uzimani. Njia nyembamba waendao ni wachache bali njia pana waendao ni wengi.
 
Hii imenikumbusha SAUT-MWANZA, masalia walifukuzwa. Wakaambiwa hata wakienda mahakamani hawatawapokea. Kwamba chuo kinaongozwa kwa mila na desturi za canon law. Hizi shule/vyuo vya kanisa ni vya kuogopa. Wanaweza kufukuza chuo kizima wakaanza upya!. Tena usije chezea warumi. Kwa mfano nimeshuhudia kosa la mwanafunzi kumpiga refa uwanjani anafukuzwa chuo, msichana kuvaa suruali unafukuzwa, kuandamana unafukuzwa. Na hii imesababisha nidhamu kuwepo.

Na seminarini ukila parachichi la paroko tu shule huna...Nidhamu kwanza. wewe unakwenda kwenye chuo chenye taratibu zake unataka uweke taaratibu zako? Kila mmoja akifanya hivyo kwa kisingizio cha UHURU WA KUABUDU na kwa jinsi hizi dini zinavyofumuka utajakuta hata wengine wanakataza kufanya kazi j3 je, tutafanyaje?.
 
sabato ni siku ya kwanza ya juma, na wala sio jumamosi, someni maandiko
Mkuu nadhani ungepitia upya maadiko. Biblia inaweka wazi kabisa kuwa jumamosi ni siku ya saba na ni sabato takatifu. Kama wewe ni mkristo unaelewa fika kuwa Biblia inaonyesha Yesu Kristo alifufuka siku ya kwanza ya Juma ambayo ni jumapili tazama Luka 24:1-3, Marko 16:9 inasema "Naye alipofufuka siku ya kwanza ya juma...."kiswahili cha kisasa imeweka wazi kabisa kuwa alifufuka siku ya jumapili. Na kama Jumapili ni siku ya kwanza, basi jumamosi ni siku ya sabato ambayo Mungu mwenyewe aliibariki, akaitakasa na kuwaagiza wanadamu wote waitunze siku hiyo kwa ibada takatifu, tazama Mwanzo 2:1-3, Kutoka 20:8-11.Wapo wnaodhani kuwa sabato ilikuwa ni agano la kale na katika agano jipya tunaokolewa kwa neema hatuna haja ya amri za Mungu. Huo ni mtazamo wa shetani ili kupotosha watu wa Mungu. Katika kitabu cha Tito 2:11,12. Biblia iansema "Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa, nayo yatufundisha kukataa mabaya". Kwa hiyo neema ya Mungu hutufundisha tutende mapenzi ya Mungu yaani kutii amri zake. Tazama 1 Yohana 5:3, na Yohana 14:15 Yesu anasema mkinipenda mtazishika amri zake.Na alisisitiza kuwa Amri kuu ni upendo na hizi amro kumi zimegawanywa katika amri 2 kuu. Amri ya kwanza ni Kumpenda Mungu kwa moyo wote ikiwa ni kutii amri zake ambazo zimeelezwa katika kitabu cha Kutoka 20 kuanzia amri ya kwanza hadi ya nne ambazo zinahusu uhusiano wetu na Mungu. Kuanzia amri ya tano hadi ya kumi zinahusu uhusiano wa mtu na mtu, ndio maana akasema amri ya pili ni kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Yesu alikuja kusisitiza waibu wetu wa kutii amri za Mungu. Tazama Mataho 5:17. "Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, la, sikuja kutangua bali kutimiliza. Kwa maana ,amin nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka. Kwa hiyo ikowa Yesu mwenyewe alitunza sabato, mwnadamu ni nani hata abadilishe? tazama Luka 4:16. Hali kadhalika mitume wa Yesu Kristo wallitunza sabato, tazama Matendo ya mitume 13: 14, 17:2. Hata katika mbingu mpya na nchi mpya bado sabato itaendelea kutukuzwa. Tazama Isaya 66: 23 "Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wnadamu wote watakuja kuabudu bele zangu, asema BWANA."Na mwisho nimalizie kwa kusema kuwa sabato itatumika kama kipimo cha uaminifu kwa watu wa Mungu na imani yao kwa Yesu kristo tunapokaribia mwisho wa wakati. Tazama Ufunuo 14:12. "Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu."Unapotafakari haya, jiulize ni nani alibadili siku ya ibada kutoka jumamosi na kuwa Jumapili? jibu liko wazi: ni kanisa la rumi wakati wa utawala wa mfalme Constantine mnamo mwaka 313 A.D. wakati huo alijifanya mkristo akajiunga na kanisa la rumi na kufanikiwa kushawishi kanisa lifanye mabadiliko ya ibada toka jumamosi hadi jumapili ambayo iliitwa siku ya jua yaani "Sunday" na wakati huo warumi waliokuwa wapagani walikuwa wakiabudu jua kama mungu wao na waliamini siku ya jua ndipo wanapokutana na "mungu wao".
 
Kwanza kabla ya mjadala kuendelea, ningependa kujua ni vitu gani ambavyo si ruhusa kwa SABATOS kuvifanya siku ya jumamosi, tukisha jua hilo then, tutaweza kuuweka mtihani katika kundi gani, baadae kutoa maamuzi, karibu..
Msabato haruhusiwi kutoka jasho na asitembee umbali zaidi ya jiwe litakapododoka baada ya kulitupa toka mlangoni kwake. Ukiwa Dar kuna joto na mtu anatokwa na jasho bila hata ya kutoka nje, hivyo ni dhambi. Kama mtu anatoka nyumbani kwake hadi kanisani ambapo ni mbali na kwake, anatenda zambi. Hivyo kama kuna mazambi hayo mengi itakuwa ni upuuzi kutofanya mtihani ati utatenda dhambi
 
Ufunuo wa Yohana 13:1-18
Inaongelea Mnyama........Papa
 
Mazee na waislamu nao wakikataa kufanya mitihani siku ya ijumaa mambo yatakueje. Principle yupo makini sana, kafanya la maana sana, sie wakristu wa jumapili mbona siku za jumapili huwa tunapiga kura.
 
Msabato haruhusiwi kutoka jasho na asitembee umbali zaidi ya jiwe litakapododoka baada ya kulitupa toka mlangoni kwake. Ukiwa Dar kuna joto na mtu anatokwa na jasho bila hata ya kutoka nje, hivyo ni dhambi. Kama mtu anatoka nyumbani kwake hadi kanisani ambapo ni mbali na kwake, anatenda zambi. Hivyo kama kuna mazambi hayo mengi itakuwa ni upuuzi kutofanya mtihani ati utatenda dhambi
Acha upotoshaji, Muogope Mungu.Tazama Ufunuo 22: 18, 19. "Na mtu yeyote akiongeza au akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima..."
 
Acha upotoshaji, Muogope Mungu.Tazama Ufunuo 22: 18, 19. "Na mtu yeyote akiongeza au akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima..."

Hata akisoma Mathayo 5:17-19 inaonesha vizuri tu
 
Acha kutuchokoza WAISLAM tumejinyamazia kimya,wakati nasoma undergraduate miaka ya 2000 mwanzoni nimefanya quiz,test na UE nyingi sana tu siku za ijumaa pale SUA.

mkuuu hajanielewa hapo mkuu,siyo kama nawachokoza waislamu ,no lengo langu nilikuwa nataka kusema kwamba siku zote iwe jumapili,jumamosi au ijumaaa, na siku zingine a,bazo wapagani waanaabudu. Chuo kama chuo kisiegamie upande wowote mkuu. mtu yoyote aweze kufanya mitihani regardless siku yake ya kuabudu
 
waache ujinga bwana.....wakiumwa hawataenda hosp siku za sabato......WALISHAAMBIWA YA KAISARI MUACHIE KAISARI NA YA MUNGU MPE MUNGU
 
Acha upotoshaji, Muogope Mungu.Tazama Ufunuo 22: 18, 19. "Na mtu yeyote akiongeza au akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima..."
Naona hujaijua dini ya Sabato!!! Jitahidi kutafuta ukweli
 
Nikirejea Ibara ya 19 ya Katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977 inatoia Uhuru wa Mtu Kuabudu.......

Hali kwa Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji ni Tofauti kwani wanafunzi wapatao 8 wamefukuzwa Chuoni hapo kwa madai ya kutofanya mitihani iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Sabato kwamba kwa kanuni za Chuo hicho hiyo si sababu ya kumfanya mwanafunzi asifanye mitihani

Wanafunzi hao wapo mitaani kwa sasa wakisaka msaada wa kisheria

  1. Je yamkini wakati wanafunzi hao wanapokelewa hilo halikuwekwa bayana?
  2. Mbona Mitihani isiwe Jumapili?
  3. Wapi Uhuru wa Kuabudu kwa mujibu wa Katiba JMT na sheria?

Je mnawashauri nini wanajamvi?
kwanza nawapa pole wapendwa kwa kusimishwa chuo! ila wasikate tamaa,maisha yanaendelea, kama wamesimama imara naamini haya ni mapito tu! mimi nilipitia sana sekondari kwenye somo la civics mwalimu alikuwa anafundisha jumamosi tu but nilikuwa best performer wa hilo somo!

vilevile wakati nasoma chuo cha usimamizi wa fedha nilikutana na hiyo changamoto lakini MUNGU alizidi kuwa mwema kwangu,naingia first year mitihani siku ya sabato ilifutwa na management ya wakati huo.kitu cha ajabu nilipomaliza mitihani ilirudishwa tena!then ata kazini nipo kitengo ambacho sifanyi kazi siku ya sabato ata ikitokea dharura management wanajua kuwa mimi ni muadventista msabato!

ushauri wangu kwa hao vijana wamkabidhi MUNGU jambo hili afanye sehemu yake!saa nyingine tukitumia ubinadamu hatutaweza.Mimi nitawasaidia kuombea jambo hili
 
Yesu aliletewa wagonjwa siku ya sabato akawaponya,wale Mafarisayo walipomlalamikia aliwapa mfano akisema,ng'ombe wako akiangukia shimoni siku ya sabato utamuacha afie humo au utamtoa?nina maana hii hao madogo wasichanganye madesa kama wapo chuo kwaajili ya kusoma wanatakiwa kusoma na si kufuata itikadi za kidini,WAMECHEMKA KWA HILO
 
wapumbavu hao wao walipokuwa wanafanya aplication TEKU hawakujua ni chuo cha dhehebu gan kwann wasingeenda kweny chuo chao arusha university ambacho kinatukuza sabato,kwanz din na elim ni tofaut j'mos ni siku ya kaz na siyo ya kuabudu!

mmh..hapo kwenye red, nafikiri ungepunguza ukali wa maneno.Japo, mm sina interest na TEKU lakini kama Bina-damu nafikiri it's unfair to call those students such a name! pia Elimu na Dini vinauhusiano.ndio maana hata Mithali inasema...watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...! Kwa uzoefu wangu nikiwa pale UDSM, ni jukumu la wangu wanafunzi kumtuma class rep. aongee na Lecturer ili kusogeza siku ya Test/U.E mbele au nyuma kama inagongana na siku ya sabato. Japokuwa kuna baadhi ya malecturer walikuwa wanagoma kufanya hivyo kutokana na shortage ya Venue. MWISHO kwa muda wangu wote pale UDSM sijawahi ona mwanafunzi anasusia U.E coz imefanyika Jmos.
 
Kuna jamaa yangu ni msabato na anaishi na demu wake geto moja.linapofika swala la kufanya mitihani au presentation jumamosi alikua anagombana sana na ma doctor. siku moja nikamwambia mbona unaishi na mwanamke na mnazini huoni hiyo ni dhambi au dhambi ni kufanya kazi jumamosi?amenichukia mpaka leo.wakati mwingine haya mambo ya imani tunajichanganya sana.
Wanachuja ngamia na kukamata mbu!
 
ni siku yao ya kuabudu.labda kuanzia jioni ya 12 ndio mtiahni unaweza fanyika. hiyo ilikuwa kawaida katika udsm chuo kongwe jumamosi test na mitihani ni usiku au jion kabisa.TEKU wanatapatapa watawarudisha hao

Hakuna kitu kama hicho wewe, UDSM test zinafanyika hadi X-Mass.
 
mmh..hapo kwenye red, nafikiri ungepunguza ukali wa maneno.Japo, mm sina interest na TEKU lakini kama Bina-damu nafikiri it's unfair to call those students such a name! pia Elimu na Dini vinauhusiano.ndio maana hata Mithali inasema...watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...! Kwa uzoefu wangu nikiwa pale UDSM, ni jukumu la wangu wanafunzi kumtuma class rep. aongee na Lecturer ili kusogeza siku ya Test/U.E mbele au nyuma kama inagongana na siku ya sabato. Japokuwa kuna baadhi ya malecturer walikuwa wanagoma kufanya hivyo kutokana na shortage ya Venue. MWISHO kwa muda wangu wote pale UDSM sijawahi ona mwanafunzi anasusia U.E coz imefanyika Jmos.

They deserve it
 
Na seminarini ukila parachichi la paroko tu shule huna...Nidhamu kwanza. wewe unakwenda kwenye chuo chenye taratibu zake unataka uweke taaratibu zako? Kila mmoja akifanya hivyo kwa kisingizio cha UHURU WA KUABUDU na kwa jinsi hizi dini zinavyofumuka utajakuta hata wengine wanakataza kufanya kazi j3 je, tutafanyaje?.

Hahahaaa...ulisoma kitalu gani ndugu ?Maua? au Uru?hapo kwenye Blue umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka nikiwa O'level nilipangwa kwenye kitengo cha Orchard(Fruits) nilikoswa[SUP]2 [/SUP]na Disco hivi[SUP]2 [/SUP]kisa Avocardo!! Lazima ufuate taratibu nyumbani kwa watu.Lakini ktk hicho chuo its too much coz hata malecturer wao walikuwa wanalazimishwa kuhudhuria ibada hata kama si wa dhehebu husika
:first:
 
Back
Top Bottom