Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
Wanafunzi wa Kitanzania walio katika mji wa Sumy nchini Ukraine wameruhusiwa kutoka nchini humo kupitia mpaka wa Russia baada ya mazungumzo ya kidiplomasia kufanyika na Serikali ya Russia kuridhia.
Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa leo Machi 4, 2022 na Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, shughuli ya kuwatoa wanafunzi wote kutoka Sumy hadi kwenye mpaka wa Russia, litaratibiwa na Serikali hiyo na tayari imeanza mipango ya utekelezaji.
“Wanafunzi hao watakapofika mpakani, Ubalozi wa Tanzania nchini Russia utawapokea kwa taratibu nyingine za kurejea nyumbani,” inaeleza taarifa hiyo ya Balozi hizo.
Taarifa hiyo inaeleza kwamba wakati shughuli ya kuwatoa wanafunzi walioko Sumy ikiendelea kuratibiwa, Balozi zinaomba wanafunzi hao pamoja na wazazi kuwa wavumilivu ili kuhakikisha wanatoka kwa usalama nchini Ukraine.
Mwananchi
My take:
Huu ndio uzuri wa kutofungamana na upande wowote, tungejifanya kiherehere hawa vijana wangepata shida sana. Huu mji wa Sumy upo mpakani wa Russia na Ukraine, ni mbali sana kuyafikia mataifa ambayo yanapokea wakimbizi wa Ukraine.