DOKEZO Wanafunzi wa kitongoji cha Njoka wasaidiwe mazingira rafiki ya kupata elimu

DOKEZO Wanafunzi wa kitongoji cha Njoka wasaidiwe mazingira rafiki ya kupata elimu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kitongoji cha Njoka kinapatikana katika Kijiji cha Kizuka wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma. Wanafunzi hawa wanakumbana na hadha kubwa sana ya kutembea takribani zaidi ya km 10 kuzifuata shule ya msingi Kizuka.

Lakini kitongoji hiki kinapakana na Kijiji cha Miembeni ambacho kipo takribani km 3 tu na kina Shule ya msingi Miembeni ambayo ipo wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma.

Wanafunzi wa Njoka hawaruhusiwi kusoma katika Shule ya msingi Miembeni kwa sababu wazazi wao ni wakazi wa Wanafunzi hawa wanakumbana na hadha kubwa sana, kutembea umbali mrefu, utoro uliokithiri, hatari ya kushambuliwa na wanyama wakali kwani eneo kubwa lina msitu mkubwa.

Hivyo mamlaka husika zisaidie kumaliza tofauti zilizopo baina ya vijiji hivi ili kuwasaidia watoto wapate elimu karibu na mazingira ya nyumbani kwao.

Mheshimiwa Jenista Mhagama pia aangalie namba ya kuwasaidia watoto Hawa maana amepelekewa malalamiko haya lakini hayafanyii kazi.

IMG_20241106_152211_531.jpg
 
Back
Top Bottom