Wanafunzi wa ngao combat wamegawanyika katika vikosi vitafu

Wanafunzi wa ngao combat wamegawanyika katika vikosi vitafu

Joined
Mar 30, 2020
Posts
68
Reaction score
106
1. Kikosi cha kwanza ni (yellow section - kikosi cha njano ) kikosi hiki ni cha wanafunzi wapya ambao wapo katika daraja la ( junior level ). Sawa na kiwango cha awali.
Kikosi hiki ni cha wanafunzi wapya wanaojiunga na mfumo wa ngao combat, lengo kuu la kikosi hiki nikumjenga mwanafunzi utayari wa kiakili na kimwili ( physical fitness and mental alertness ).

MAFUNZO
Mafunzo ya Kikosi hiki yanajikita katika kanuni ya ( awareness - utambuzi ) wanafunzi wanafundishwa namna yakusoma mazingira yao, kutambua hatari mapema kabla haija tokea na jinsi ya kuiepuka hatari hiyo, pia wanafundishwa jinsi ya kusimama pindi wanapo kuwa katika mapigano, mbinu za msingi za kushambulia, kuzuia, maeneo hatarishi ya kumpiga adui, mazoezi ya viungo, miondoko ya kukwepa pamoja na mbinu za msingi za kujinasua ( escapes ) pindi anapo vamiwa na kushikwa au kukabwa ghafla na muhalifu.

2. Kikosi cha pili ni ( blue section - kikosi cha bkuu ) kikosi hiki ni cha wanafunzi wakongwe, ambao wapo katika daraja la ( senior level ). Sawa na kiwango cha kati / juu.

3. Kikosi cha tatu ni ( green section - kikosi cha kijani ) kikosi hiki ni cha wakufunzi ambao wapo katika daraja la ( master level ) sawa na kiwango cha ukufunzi / utaalamu, hii ndio ngazi ya juu kabisa na ya mwisho katika mfumo wa ngao combat .
 

Attachments

  • SGN_11_03_2026_1793678890669.png
    SGN_11_03_2026_1793678890669.png
    1.1 MB · Views: 1
Back
Top Bottom