JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Nimesoma uzi wa wanafunzi flani huko Singida wampata msala wa kukamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kuchoma moto pikipiki ya mwalimu na kufyeka shamba la mwalimu huyo baada ya kumpa adhabu mwanafunzi mmoja aliyekutwa na simu.
Mwanafunsi huyo ni wa sekondari, binafsi hata mimi siungi mkono mchongo waliofanya hao wanafunzi, mimi nauita ni usela feki wa ujanani.
Lakini hoja ya msingi wadau tujadiline, hivi ni sahihi kweli kwa levo ya sekondari wanafunzi kutoruhusiwa kuwa na simu?
Dunia ya sasa kweli simu inazuilika? Nimewaza kwa nini simu wawe nazo lakini kuwe na masharti maaluma ya kutumia mfano kutotumika darasani au wakakti wa shughuli za shule, au labda wawe wanaenda nazo shuleni kisha zinakabidhiwa kwa uongozi wakati wa wikiendi wanakabidhiwa ili wawe wana focus na masomo siku za katikati ya wiki.
Mnaonaje hili wadau......