Tatizo sio simu,shida ni self control za wanafunzi wenyewe na kujua umuhimu wa kutumia hizo simu wakiwa shuleni, tusiangalie tu madhara ,kutumia simu pia kuna faida zake vilevile.
Binafsi naona kama kweli simu zikitumika vizuri zinaweza kuleta faida kama ilivyokusudiwa.
Tumechelewa sana kuamua hili.
Humu duniani hakuna kisicho na madhara.
Naona nguvu inayotumika kuzuia simu ni kubwa mno kuliko kama ambavyo tungeruhusu zitumike kisha tuangalie namna ya kudhibiti madhara.
Nashangaa ninapoona mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne akichaguliwa kuingia kidato Cha tano anaambiwa haruhusiwi kutumia/kumiliki simu wakati mwenzie waliyehitimu pamoja kidato Cha nne aliyechaguliwa kwenda chuo Cha kilimo, mifugo, uhasibu, VETA na kwingineko anaruhusiwa kutumia simu.
Huko nyuma ilizuiwa kuweka redio kwenye magari kwa hofu kuwa madereva watasababisha ajali kwa kusikiliza redio au muziki.
Nakumbuka miaka michache iliyopita, haikuruhusiwa kusogelea benki baada ya saa 12:00 jioni. Leo hali ikoje?
Kwenye familia nyingi wazazi/walezi hatuwapi simu wanetu.
Ajabu ni kuwa tunapotatizika kutumia simu zetu, wao ndio wanatuelekeza tufanyeje.
Wao ndio wanafahamu walikojifunzia namna ya kuzitumia.
Hatuna uwezo wa kuunda dunia yetu.
Wenzetu wanakabilije hali hii?