Unahitaji kupata elimu ya kujitambua, na huelewi hata unachobishia so unaishia kuattack personality badala ya kujadili hoja na kutoa point zinazotetea unachozungumzia.
Tuache ushabiki, kama wewe ungebahatika kupata Div 1 ya pt 3-7 ungesoma chuo gani? Jijibu kimoyomoyo hafu useme ukweli, tafuta HRs waulize kwenye Database yao chuo gani wanakirank no moja wanapoajiri kutoka vyuoni moja kwa moja.
Kwa taarifa yako ni kozi moja tu hapa Tanzania iliyoweza kushindana na kozi za UDSM, naizungumzia BAF ya Mzumbe. Atleast hii unaweza ukawakuta watu wenye Div 1 ya 3 na 4 wachache. Tofauti na hapo watu wote waliofaulu vizuri wanajiunga UDSM.
Kwa wanaosoma kozi za biashara watanikosoa hapa: UDSM ni chuo ambacho kimekuwa kikiongoza mara nyingi zaidi ya vyuo vingine kwenye mitihani ya NBAA.
BIG 4 (pwc, EY, Deloitte na KPMG) zinaajiri more than 60% kutoka UDSM (hapa nazungumzia vyu vya ndani tu), na haya ni makampuni ambayo sera zao ni kuajiri watu wenye uwezo mkubwa kiakili na matokeo na wanaofundishika kirahisi.
Watu wanawalalamikia sana graduate wa UDSM kwamba ni wasumbufu hasa kwa sababu hawakai sehemu moja kikazi, wako marketable na wanaijua thamani yao.