Wanafunzi wa vyuo vikuu mkue jamani acheni utoto!!!


Nisome vizuri tena...kuna mahali nimesema kuwa na utaratibu wa kiserikali wa kupata laptops hizi kwa bei nafuu na kama hakuna uwezo wa kuwapa bure basi iwakopeshe!...hapa tatizo linatoka wapi? Ni suala la priorities na ufisadi tu ndio linalotusumbua nchi hii. Haya mambo tunaona hayawezekani lakini kwa hakika tunayo potential ya kutoa hizo laptop kwa kila mwanafunzi, tena bure. Tatizo la Tanzania sio uwezo hasa ni namna tu tunavyofikiri! Cha muhimu hapa ni je laptop ni muhimu kwa mwanafunzi wa sasa wa chuo kikuu? Kama jibu ni ndio basi serikali haina budi kuweka utaratibu mzuri wa kuwezesha upatikanaji wake. Mimi naona sio muhimu tu ni suala la lazima!
 
Pdidi nakubaliana na kauli zako,angalia jinsi mwanachuo mmoja alivyokujibu hapa chini, unaweza ukacheka au ukalia
usilaumu sana nahisi alioandika hii thread kasoma coarse ambazo special faculty req haina umuhimu so muambie afufuke sababu tayari ashakufa..
 

kwa hyo Pinda alitoa ahadi ili kuwaridhisha?
 

umeongea vyema, kwa mfano serikali ingeweza kufanya tax exemption na ingekuwa rahisi hata kwa chuo kununulia wanafunzi wake laptops na hiyo pesa wangeifix kwenye ada.
Sio tu udom, kuna baadhi ya kozi katika vyuo vyote wanahitaji pc.
Nawashangaa wanaoona hili jambo ni gumu.
Nafikiria hata kungekuwa na utaratibu ukiingia chuo unapewa laptop ukigraduate unarudisha.
Nishaona tz hatuendelei maana mambo mengi huwa tunaona hayawezekaniki. Hatuna hata ule moyo wa kuthubutu.
 
Mpaka sasa hivi computer na vitu vyenye uhusiano na computer vinaexemptions hasa kwahiyo hata ukitaka kutoa nafuu kwenye kodi sijui ni nafuu ipi tena. Priorities kwa sasa ni kuelekea kwenye IT kwa nguvu yote lakini si kwa kugawa laptop. Mie bado nasisitiza uwepo wa library computer kama sehem nyingine duniani ziweze kutumia na wanafuzni wote na kama somo lao ni muhim kihivyo yaani wanahitaji computer maalum basi iweke library ambayo wanafunzi wa mwaka wa 1-3 watatumia. Ni lazima tufikiria namna ya kupunguza matumizi kwa serikali lakini si kuongeza matumizi. Hebu leo hii tuweke hesabu rahisi; wanafunzi wanaosoma elimu ya juu; labda 50,000 X 1000000= ni bil 50. Bado hujawapa mkopo. Unless kama serikali inasomesha tu, hospitali na barabara hazijengwi. Tuwafundishe wanafunzi hawa kujitegemea. Pia kwenda kukopa ni ishu maana Watz hawana culture ya kulipa. Ukimkopesha mwanafunzi ndio imetoka hiyo. Nadhani unajua mabilioni ya JK nk. Nami nisistize, computer ni muhim (si lazima laptop), ila iwepo sehemu ambayo itaendelea kuwa mali ya chuo na itatumika na wengi kwa kipindi kirefu.
 
Hivi ukiingia chuo ukapewa laptop baada ya miaka 3 unairudisha, inakuwa bado laptop hiyo?
 
Mpaka sasa hivi computer na vitu vyenye uhusiano na computer vinaexemptions hasa kwahiyo hata ukitaka kutoa nafuu kwenye kodi sijui ni nafuu ipi tena.
Ndio maana nikasema serikali inaweza kuingia mikataba na manufacturers ili bei iwe chini zaidi pamoja na kutokuwapo kwa kodi.

Unakwendaje kwenye IT bila computer? Kwenye baadhi ya vyuo hizi comp labs zipo lakini ni kama hazina mwenyewe. Unakuta nusu ya computer hazifanyi kazi!

... Ni lazima tufikiria namna ya kupunguza matumizi kwa serikali lakini si kuongeza matumizi. Hebu leo hii tuweke hesabu rahisi; wanafunzi wanaosoma elimu ya juu; labda 50,000 X 1000000= ni bil 50.
Tupunguze ufisadi kwanza....hilo ndio tatizo letu kubwa. Kuna mabilioni yanapotea kwenye ufisadi, sembuse hiyo bilioni 50 kutumika kuwakopesha/kuwapa laptops wanafunzi? Tizama tu magari na matumizi mengine ya watu tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Kumbuka tunaokataa kuwapa laptops ni watanzania!

Msome kidogo huyu jamaa hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/133791-nimeharibu-siku-yangu.html

...Tuwafundishe wanafunzi hawa kujitegemea....
Huwezi kuwafundisha kujitegemea kwa kuwanyima nyenzo muhimu katika kupata elimu yao! Sana sana utawafundisha kutoyapa umuhimu unaostahili masuala ya elimu...kumbuka hawa ndio watakuja kuwa watendaji wa baadae katika serikali na kwengineko. Kama kuwanyima nyenzo ndio kutawafundisha kujitegemea basi hata nyenzo nyingine kama meza madarasani zingeweza kutolewa tu ili wakae chini ('watie akili'!).

..Pia kwenda kukopa ni ishu maana Watz hawana culture ya kulipa. Ukimkopesha mwanafunzi ndio imetoka hiyo. Nadhani unajua mabilioni ya JK nk. ...

Hapa sijakuelewa unataka kusema nini! Wanafunzi hawakopeshwi kwa ajili ya kufanya biashara...bali kuweza kusoma na wanategemewa walipe baada ya kumaliza chuo. Binafsi bado nalipa mkopo niliopewa kwa ajili ya chakula na malazi.

..Nami nisistize, computer ni muhim (si lazima laptop), ila iwepo sehemu ambayo itaendelea kuwa mali ya chuo na itatumika na wengi kwa kipindi kirefu.
At least we can partly agree on this...linataka kufanana na wazo alilotoa Husniyo hapo juu, ingawa naona umelipinga kwenye post yako hapo juu!
 


Uninafsi wa watanzani unaanzia mara wakifika kwenye vyuo vikuu.sasa ubinafsi wa wanafuzni wa Vyuo vikuu ni sawa na wa wabunge.

wanasahau walipotoka .....
Hawaandamani kutetea maslahi ya wakulima , wafanyakazi amabo bila wao hizo pesa hazipatikani.

Kesho utasikia wahadhiri mamegoma. keshoutwa madokta. Ila siku wakulima wakiwa na umoja wakagoma ndo tutajua umuhimu wao. Ukweli ni kwamba ukishafika chuoni unajifunz kuwa selfish. Nicho wanachofanya wanafunzi. From there on ndo baadae zinakuja kagoda, EPA
, and the like

Serikali ishukuru wakulima hawana umoja.
 
Wazee wao wananyanyasika vijijini waowanadai laptop!!Ndizo zinazofundisha?

Si tu azifundishi,pia uwezi sema special facult requirements,ni sawa na mimi wakati uleeeeeeee!Lizzy nidai excavator kama special facult requirement.

Kuwa na computer kwa kila mwanafunzi wa elimu ya juu ni muhimu! na sio lazima laptop!kwa kuwa uchumi wa nchi ni mdogo basi wangeomba ata computer labs. za kutosha ili kila mtu kwa mda wake anaweza kujifunza.

Nacho amini ata ukiwa na laptop yako kwenye iyo kozi unaosoma sio kila mara utaitaji iyo computer kuna masomo mengine pia.

Ushauri wangu vijana wakue!walete madai ya msingi na sio bla bla tu.
 
Ni vema sasa hata wananchi baki wameanza kuwastukia hawa 'wasomi' wetu. Inaonekana siku hizi vyuo vyetu vina-enroll makundi ya wahuni badala ya scholars. Kha!
 
.
Kuwa na computer kwa kila mwanafunzi wa elimu ya juu ni muhimu! na sio lazima laptop!

nafikiri wameomba laptops kwa sababu ya urahisi wa kubeba na kujisomea mahali popote mtu angependa.
Unaweza ukabeba desktop ukaenda nayo darasani?
 
Hivi ukiingia chuo ukapewa laptop baada ya miaka 3 unairudisha, inakuwa bado laptop hiyo?

kumbe inakuwa dala dala jamani?
Mashine ngapi zinadumu zaidi ya miaka hata 5? Inawezekana hata vifaa vyako vya ofisini vina zaidi ya hiyo miaka.
Kwa wazo nililotoa kumbuka haitokuwa hasara kwa chuo wala gvt kwasababu gharama ya laptop itakuwa inalipiwa kwenye tuition fee ya mwanafunzi kidogo kidogo hadi anamaliza. Kwa mfano
Kama tuit fee ya mwanafunzi ni laki 5, anaweza kulipia lak 7 ambapo lak 2 itacover gharama ya laptops.
Ni suala la serikali na vyuo vikuu kutengeneza strategies nzuri za kuwezesha hilo jambo bila kuumiza upande wowote.
 
kumbuka kunanchi kama rwanda wanakauli mbiu ya one student one laptop na imewezekana,


kwanini tz ishindikane!
Sijaelewa kwa nini watu wanapinga hili wazo kwa nguvu zao zote.
 
kwa wanavyuo kupewa laptops ni sahihi na serikali inaweza weka mpango maalum wa kuwapa vijana laptops za bei ya kawaida na kuwakata kwenye posho zao mbalimbali hadi deni liishe......ni sera tu hakuna ...,,,vilaza wamejaa serikalini hadi bodi kwenyewe hamna anaefikiria................we unaesema wajengewe maabara huo utitiri wa wanafunz vyuoni utawasev vipi na izp pc...si itakua ugomv na ukizingatia most of the times wanafunz wanasoma usiku....

tofaut na hapo siwatetei sana maana ata mimi mwenyewe nilianza na pc ya kuasemble kkoo laki 2.50 second yr third year nikaiuza nikanunua laptop ya laki 4.50...na niliish mtaani na sikutegemea fungu LOLOTE zaidi ya ZE BOOM...punguzeni beeeer wik ya 1 hadi ya 4
 
This is why I like JF. Maana at the end of the day ufumbuzi wa matatizo yetu unapatikana kupitia hoja. Sinatatizo na serikali kuingia mkataba na manufacturers, tatizo ni nani wa kununua hizo computer. Serikali ijenge mazingira ya kufanya computer zitumike na wengi. Sijaelewa unamanisha nini kwamba unakwenda comp library, then comp zaidi ya nusu hazitumiki. Ni mbovu au hakuna watumiaji. Kama suala ni ubovu basi hapo kuna tatizo maana zinahitaji usimamizi. Sehem mbalimbali duniani wana hizi comp library na wanachofanya ni kuhakikisha zote zinafanya kazi, zipo well secured, wanafunzi wanaaccess na wanasaidiwa pia pale wanapokuwa na matatizo kwenye comp lab.
Ufisadi ni tatizo, kila mtu anafaham lakini wakati tuandelea kupunguza ufisadi lazima tuhakikishe mambo mengine yanakwenda. Kutowapa laptops si kutowanyima nyenzo muhim. Nimesema na ninasema tena, kugawa laptops hakutaweza kuwa sustainable kwa uchumi wetu. Sijui kama unakumbuka vyema, zamani vyuoni walikuwa wanagawa calculator lakini baadae waliacha na mambo yaliweza kwenda. Hivi bilioni kama 50 tukiwekeza kwenye kilimo, barabara au training ya walimu au kuboresha shule za kata unadhani kwa miaka 5 kitatokea nini? Hivi priority ya sasa ni kugawa computer kwa wnafunzi wa vyuo vikuu. Au kwakuwa wao wanayosehem ya kusema na nirahisi kusikika? Hali za wanafunzi wa level za chini zikoje?
Hapo kwenye nyenzo muhimu, sijasema wanyimwa bali chuo kiwe na library ya kueleweka ya computer na computer moja itumike kwa mass training na si individual. Kugawa laptop that will be beyond government responsibility. Hoja ya Husninyo inatofautiana na yakwangu. Yeye anasema wapewe wanapomaliza warejeshe, mie ninasema ziwepo library za computer na wanafunzi wafanye kazi zao hapo ili computer moja itumiwe na wanafunzi wengi.
 
Hawa wanafunzi wanalalamika posho haiwatoshi unawakata kwenye posho ipi? La maabara/library ya computer mbona linawezekana na linafanyika? Hivi unadhani hao wote wanaodai hiyo computer watakuwa maktaba muda wote. Pia si wote wanasoma usiku na haishindikani kufanya hiyo comp lab kuwa 24 hrs, suala ni kuamua.
 
nafikiri wameomba laptops kwa sababu ya urahisi wa kubeba na kujisomea mahali popote mtu angependa.
Unaweza ukabeba desktop ukaenda nayo darasani?
Kwenye elimu issue za conviniency ni individual based. Bado kidogo wataanza kudai video training/conferencing kama ndio hivyo. Kinachohitajika na mazingira muafaka sehem za kusomea na si kuanza kugawa laptops, pen, suruali, shati nk. Maana ndio tunakoelekea.
 
Husninyo hivi unajua ni mkopo kiasi gani wa elimu ya juu umelipwa mpaka sasa. Yaani mie natamani wakulima washtuke na wao juu ya madai ya wenzao yasiyo endelevu kwa nchi nzima. Kila mtu ana namna ya utunzaji na utumiaji wa vifaa. Kuna mwingine atainstall program weee at the end of the day computer inakufa. Ukiweka maabara kuna kuwa na restrictions za installations na utunzaji na vitu vinadumu. Tena unaweza kuweka security camera tu, akawepo mtu mmoja au wawili kwenye control room then wanafunzi wakaendelea kijufunza na kusave gharama. Mie sina tatizo na wao kujifunza ila ni vyema tuwe tunatoa ushauri ambao unafikiria na sekta nyingine zinazohudumiwa na serikali.
 
Mmmm!!!unajua kuna mada nyingine ukiisoma ni nzuri sana,lakini wachangiaji sasa ndo wananiacha hoi,soma wote walochangia thread hii utanisoma.
 
naunga mkono hoja kuhusu computer libray. Je zipo vyuoni? Kuna computers za kutosha na wasimamizi wa kutosha!?
Tuassume kozi yenye wanafunzi mia 5 ambao wanahitaji kuelekezwa moja kwa moja kwa kutumia computer, je wakasomee library?
Jibu hapo ni ndio na library lazima iwe na computers mia 5 ili kila mmoja awe na yake. Sasa, kwa muda ambao hao wanafunzi wapo comp lab wanasoma ina maana wanafunzi wengine wasiingie library kwahiyo ratiba ya wengine imevurugika.
Wote tunajua chuoni sio kama primary au secondary kwamba wote mnafika shule, mnakaa assembly. Kengele inagongwa mnaondoka kwa pamoja.
Vyuoni hakuna ratiba sawa na hapo ndipo utaona kuwa kuwa na pc ni muhimu kwa hawa mastudents.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…