SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,889
SMU idea yako ni nzuri lakini si endelevu. Hawa wanafunzi wanaingia chuo kila mwaka. Kwahiyo serikali kila mwaka iwe inanunua laptops? Mie nadhani wao kama hawana vitu vya kufundishiwa kama Maabara ingekuwa rahisi kuelewa tatizo ni nini. Hivi kweli katika elimu yetu priority inaweza kuwa laptop kwa wanafunzi wa Informatics? Umuhimu wa ICT unafahamika tena kwa kila mtu, kununua computer ni moja ila cha msingi professional yoyote inahitaji jitihada binafsi kujiendeleza. Vinginevyo, wanaosoma kilimo watadai matrekta muda si mrefu na wale wa mifigo sijui watadai nini au wanapewa nini. Tujifunze kujitafutia uwezo na si kuwa tegemezi.
Nisome vizuri tena...kuna mahali nimesema kuwa na utaratibu wa kiserikali wa kupata laptops hizi kwa bei nafuu na kama hakuna uwezo wa kuwapa bure basi iwakopeshe!...hapa tatizo linatoka wapi? Ni suala la priorities na ufisadi tu ndio linalotusumbua nchi hii. Haya mambo tunaona hayawezekani lakini kwa hakika tunayo potential ya kutoa hizo laptop kwa kila mwanafunzi, tena bure. Tatizo la Tanzania sio uwezo hasa ni namna tu tunavyofikiri! Cha muhimu hapa ni je laptop ni muhimu kwa mwanafunzi wa sasa wa chuo kikuu? Kama jibu ni ndio basi serikali haina budi kuweka utaratibu mzuri wa kuwezesha upatikanaji wake. Mimi naona sio muhimu tu ni suala la lazima!