Tanzania kwa sasa inatatizo la walimu na kitu cha kushangaza serikali inasomesha wanafunzi wengi kwenye vyuo vikuu ambao hawatalipa mikopo yao. Mimi ningeshauri serikali kwa wakati huu wa uhaba wa walimu wange weka ulazima wa wanafunzi wa vyuo wa mwaka wa mwisho kufundisha kwa miezi sita tu kabla ya kupewa vyeti vyao. Inashangaza watanzania tunafikiria kila kitu serikali ifanye, lakini serikali inatakiwa kuweka sera kwa Watanzania kusaidiana wenyewe sioni sababu ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni kwanini wasifundishe kwa sasa wakati serikali inafanya mikakati ya kusomesha walimu.
Tutapiga siasa lakini kama kizazi kijacho hakina elimu Tanzania itatawaliwa na vijana wa nje.
Tutapiga siasa lakini kama kizazi kijacho hakina elimu Tanzania itatawaliwa na vijana wa nje.