Wanafunzi wageuka kuwa wafanyabiashara Katavi

Wanafunzi wageuka kuwa wafanyabiashara Katavi

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Hali ya biashara ya vyuma chakavu na matunda mbambali inaendelea kushamiri katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi na imekuwa ikifanywa kwenye maeneo mbambali ya Manispaa hiyo na watoto wadogo ambao wanapaswa kuwa Shuleni kwenye shule za Msingi.

Licha ya Serikali kufanya jitihada kubwa za kuboresha miundo mbinu ya elimu hali ya watoto wadogo katika Manispaa ya Mpanda ni tofauti kabisa kwani muda ambao watoto hao wanatakiwa kuwa shuleni wao wanatumia muda huu kufanya biashara mitaani na kwenye nyumba za sitarehe.

Biashara ambazo watoto hao wengi umri wao ni kati ya miaka tisa hadi 13 wanazozifanya ni vyuma chakavu na matunda kama ndizi, Tango, Karanga, machungwa na maembe.

Mmmoja wa watoto hao Mkazi wa Mtaa wa Shanwe ambae jina limehifadhiwa amesema kuwa wamekuwa hawaendi shule na badala yake wamekuwa wakilanda landa mitaani kutafuta vyuma chakavu na kwenda kuviuza.

Amebainisha kuwa soko lao kubwa la kuuza vyuma chakavu lipo maeneo ya madukani kati kati ya Manispaa ya Mpanda ambapo kilo moja ya chuma chakavu wamekuwa wakiuza kwa bei ya shilingi mia tano.

Nae mtoto mwingine mkazi wa Kawajense amesema kuwa wao licha ya kuwa bado na umri mdogo kufanya biashara muda wa masomo wanaona ni jambo la kawaida kabisa kwani hakuna hatua zozote ambazo wanachukuliwa wao wala wazazi wao.

Ameitaja changamoto ambayo wamekuwa wakikutana nayo wanapokuwa wanafanya biashara za kuuza matunda na mboga mboga ni kuna wakati kuna watu wanao kuwa sawa na baba zao na wengine kupita hata umri wa baba zao wamekuwa wakiwataka kufanya nao mapenzi bila kujali kuwa wao bado ni watoto wadogo bado.
 
Nae mtoto mwingine mkazi wa Kawajense amesema kuwa wao licha ya kuwa bado na umri mdogo kufanya biashara muda wa masomo wanaona ni jambo la kawaida kabisa kwani hakuna hatua zozote ambazo wanachukuliwa wao wala wazazi wao.


Nimecheka hapa😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom