Wanafunzi Walawitiana

Wanafunzi Walawitiana

SI unit

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
1,953
Reaction score
767
Wanafunzi wa shule ya msingi darasa la 6 na la 7 wafukuzwa shule na kufunguliwa kesi mahakani baada ya kugundulika kufanya mchezo endelevu wa kuwalawiti wanafunzi wenzao.

Source: NIPASHE NEWS PAPER sunday 8/4/2012.
 
Wewe SI Unit kwanini umeileta thread hii leo? Papa ameshaomba msamaha kwa niaba ya maaskofu waliokua na tabia ya kulawiti vijana. Tusherehekee pasaka kwa amani
 
kuna uhusiano gani wa wanafunzi na kanisa?
 
Wanafunzi saba wanaosoma Shule ya Msingi Yombo Buza, jijini Dar es Salaam wamefukuzwa shule na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kutajwa na wanafunzi wenzao kuwa ni vinara wa kuwalawiti wenzao.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Steven Kailembo, aliithibitishia NIPASHE Jumapili kuhusu kufukuzwa kwa wanafunzi hao kufuatia uchunguzi uliofanywa na gazeti hili baada ya kushamiri kwa vitendo hivyo katika shule za msingi.

Kailembo aliwataja wanafunzi hao (majina tunayo), baadhi yao wakiwa darasa la saba na wengine darasa la sita, wakati mmoja wao anaendelea kufanyiwa uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.

Mwalimu Kailembo alisema Kamati ya shule imeridhia kufukuzwa kwa wanafunzi hao ili usalama uweze kuwepo kwa wanafunzi waliobaki. "Tumeona tuwafukuze kwani watu wachache hawawezi kutuharibia wanafunzi waliobaki," alisema Kailembo.

Alisema kabla ya kuwafukuza wanafunzi hao walibaini kuwa mwanafunzi wa darasa la nne ambaye ni mvulana alifanyiwa kitendo cha kulawitiwa na kuharibiwa ambapo mpaka sasa bado anaendelea kupatiwa matibabu baada ya kuharibiwa vibaya.

Kailembo alisema taarifa dhidi ya tukio hilo aliliwasilisha kwa Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke ambapo katika kipindi hicho waliagizwa maafisa elimu kulishughulikia suala hilo shuleni hapo. Alisema baada ya maafisa hao kufika shuleni hapo waliwafundisha wanafunzi kuhusu usalama wao kujitambua na kusema kitendo chochote kibaya wanachokiona au kufanyiwa.

Alisema baada ya hapo zoezi lililofuata kila mwanafunzi alitakiwa kuandika jina la mwanafunzi yeyote ambaye anajihusisha na vitendo vya kuwalawiti wenzake au kama alishawahi kufanyiwa vitendo hivyo aandike na kumtaja mtu aliyemfanyia.

Alisema zoezi hilo llilikwenda vizuri na lilianzia kwa darasa la kwanza hadi la darasa la saba.
Kailembo alisema wanafunzi 11 walitajwa katika shule nzima na kwamba walivyoendelea na uchunguzi wao dhidi ya majina ambayo yametajwa walibaini majina saba ya wanafunzi waliotajwa kuwa vinara wa kuwalawiti wenzao.

"Wanafunzi hao saba ambao wengi wao wapo darasa la saba walionekana ni vinara katika kura zilizopigwa na wanafunzi na maajabu mengine hata wanafunzi wa darasa la kwanza waliwataja katika kura walizopiga na kila darasa lilikuwa likiwataja wanafunzi hao," alisema.
 
Serikali kupitia Wizara ya Elimu tafadhari sana iangalie Kipengele kilichotolea na Rais wanacho kiita Presidential Order kuwa Wanafunzi wote Pamoja na makosa wanayo fanya,Ma afisa Elimu wahakikishe wanamaliza shule na wasifukuzwe.

Wanafunzi wanafanya mengi sana siku hizi.Niliyoshuhudia baadhi ni haya hapa walimu kupigwa, Waalimu kutukanwa nk, Wanafunzi wa leo ni hatari mno,kuanzia msingi hadi sekondari.
 
Serikali kupitia Wizara ya Elimu tafadhari sana iangalie Kipengele kilichotolea na Rais wanacho kiita Presidential Order kuwa Wanafunzi wote Pamoja na makosa wanayo fanya,Ma afisa Elimu wahakikishe wanamaliza shule na wasifukuzwe.
Wanafunzi wanafanya mengi sana siku hizi.Niliyoshuhudia baadhi ni haya hapa
walimu kupigwa
Waalimu kutukanwa nk
Wanafunzi wa leo ni hatari mno,kuanzia msingi hadi sekondari.
Mkuu hicho kipengele kipo kwenye sheria au kwenye kanuni za wapi? Na kumaliza shule kuna maana gani, la saba, form 4, form 6 au Chuo kikuu? Wote wanaosoma katika viwango nilivyovitaja hapo wanaitwa wanafunzi.
 
Wanafunzi saba wanaosoma Shule ya Msingi Yombo Buza, jijini Dar es Salaam wamefukuzwa shule na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kutajwa na wanafunzi wenzao kuwa ni vinara wa kuwalawiti wenzao.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Steven Kailembo, aliithibitishia NIPASHE Jumapili kuhusu kufukuzwa kwa wanafunzi hao kufuatia uchunguzi uliofanywa na gazeti hili baada ya kushamiri kwa vitendo hivyo katika shule za msingi.

Kailembo aliwataja wanafunzi hao (majina tunayo), baadhi yao wakiwa darasa la saba na wengine darasa la sita, wakati mmoja wao anaendelea kufanyiwa uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.

Mwalimu Kailembo alisema Kamati ya shule imeridhia kufukuzwa kwa wanafunzi hao ili usalama uweze kuwepo kwa wanafunzi waliobaki. "Tumeona tuwafukuze kwani watu wachache hawawezi kutuharibia wanafunzi waliobaki," alisema Kailembo.

Alisema kabla ya kuwafukuza wanafunzi hao walibaini kuwa mwanafunzi wa darasa la nne ambaye ni mvulana alifanyiwa kitendo cha kulawitiwa na kuharibiwa ambapo mpaka sasa bado anaendelea kupatiwa matibabu baada ya kuharibiwa vibaya.

Kailembo alisema taarifa dhidi ya tukio hilo aliliwasilisha kwa Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke ambapo katika kipindi hicho waliagizwa maafisa elimu kulishughulikia suala hilo shuleni hapo. Alisema baada ya maafisa hao kufika shuleni hapo waliwafundisha wanafunzi kuhusu usalama wao kujitambua na kusema kitendo chochote kibaya wanachokiona au kufanyiwa.

Alisema baada ya hapo zoezi lililofuata kila mwanafunzi alitakiwa kuandika jina la mwanafunzi yeyote ambaye anajihusisha na vitendo vya kuwalawiti wenzake au kama alishawahi kufanyiwa vitendo hivyo aandike na kumtaja mtu aliyemfanyia.

Alisema zoezi hilo llilikwenda vizuri na lilianzia kwa darasa la kwanza hadi la darasa la saba.
Kailembo alisema wanafunzi 11 walitajwa katika shule nzima na kwamba walivyoendelea na uchunguzi wao dhidi ya majina ambayo yametajwa walibaini majina saba ya wanafunzi waliotajwa kuwa vinara wa kuwalawiti wenzao.

"Wanafunzi hao saba ambao wengi wao wapo darasa la saba walionekana ni vinara katika kura zilizopigwa na wanafunzi na maajabu mengine hata wanafunzi wa darasa la kwanza waliwataja katika kura walizopiga na kila darasa lilikuwa likiwataja wanafunzi hao," alisema.

yaani tunasubiri mpaka watoto walawitiane ndio tunawafundisha kuhusu usalama wa kujitambua na kuripoti kitendo chochote kibaya wanachofanyiwa.

Kama shule zingekua zinatoa hii elimu mara kwa mara kwa wanafunzi labda hao watoto wasingefikia kufanyiana huo uchafu.

Inasikitisha sana maana kwa mtindo huu watoto wetu wataendelea kulawitiwa na wenzao huko mashuleni.
Inasikitisha sana.
 
siyo buza tu!!!
hata kwetu wapo.
wazazi tuwe tunawapa watoto wetu wadogo elimu kabla hawajaharibiwa-tusiache hadi walimu wagundue tutakua tumechelewa!!
ee Mungu wanusuru watoto wetu
 
kuna umuhimu wazazi kuzungumza na watoto wao kuhusu maswala haya....kabla hajaharibiwa au kuharibika mtaani....
 
Ee Mungu tuokoe na janga hili! napita njia tu wukuu, nitachangia baadae!
 
Ki_ukweli mimi sina haja ya kuiona mianafunzi dizain hii, unajua ukitaka kuhisi ubaya wa kitendo walichowatendea wadogo zao basi katoto kalikolawitiwa kawe kakwako tena kadarasa la pili
 
Wanafunzi hawa wakipata division 4 na zero tutashangaa kweli?
 
Watoto wa shule zetu za kata wanasoma kwenye mazingra hatarishi sana......uko boarding nako hali ni ile ile, zaid ni kuwaombea watoto wetu wajitambue kua wao ni jinsia gani si unaambiwa geuka nyuma lala unalala tu hatari sana
 
enzi zetu zile fimbo zinatembea shuleni huqwezi sikia upuuzi kama lkn sasa? mnasema tunalea kisasa sio? tusubiri makubwa zaidi ya haya ikiwa ni pamoja na walimu kulimwa shaba/risasi na wanafunzi we are now counting days to disaster
 
Back
Top Bottom