Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge leo Jumanne Januari 5 amesema wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu watasoma kwa zamu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya shule kwa ajili ya wanafunzi hao, Kunenge amesema wamefikia hatua,ili wengine wasibaki nyumbani na itakapofika Februari 28,2021 wataendelea na utaratibu wa kawaida.
"Tayari Mkoa umeomba kibali wanafunzi wetu wote waende shule japo kwa shift kutokana na uhaba wa madarasa ambapo wataanza Januari 11, 2021.
"Ila itakapofika Februari 28 ambapo ni agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa madarasa yawe yamekamilika na wanafunzi awamu ya pili wawe wameingia darasani wataendelea na utaratibu wa kawaida wa kwenda wote asubuhi," amefafanua Kunenge.