Jamani wana jamvi nimejiuliza maswali mengi kuhusiana hili janga la wanafunzi kukosa madarasa kwa ajili ya kujiunga kidato cha kwanza nimebaki najuliza majukumu ya wizara kwa sasa ni kutanga matokeo ya mitihani ya kitaifa tuu na ufanyikaje wake?...
Mimi najiuliza hivi:
Wizara ya Elimu ina
1. Maafisa Elimu Mkoa
2. Maafisa Elimu Wilaya
Ambao kazi yao kubwa ni Ku coordinate Maswala yote ya Elimu.
Ongezeko la Watoto kwa mfano kwa mwaka huu lilijulikana tokea Enrollment yao wakiwa Darasa la Kwanza; Mtihani wa kuvuka Darasa la 4.
Sasa hawa Maafisa Elimu walikuwa wapi ku oversee na Kumitigate hili Tatizo.
Mpaka Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI kuamua kuingilia Kati.
Ina maana kila Mwaka hali itakua ndio hivi hivi?
Ingekua ni kwenye Financial Institutions ambazo zenyewe ni Matokeo ni Faida au Hasara ( Profit or Loss) ina maana Makampuni karibu yote yangeshapata Hasara kubwa sana kutokana na kushindwa kwa Managers ku forecast and Ku-Mitigate Risks!!!
Kila Mwaka Sekta ya Elimu ( Msingi na Sekondari) zimekua na Matatizo ya Zimamoto katika
1. Upungufu wa Vyumba vya Madarasa
2. Upungufu wa Viti vya Kukalia
Ni wakati umefika Wahusika kujirekebisha kwa mapungufu yao.
Kama tatizo ni Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri basi ikiwezekana idara za Elimu zirudishwe katika Wizara Husika kama Miaka ya Zamani.