KERO Wanafunzi wanaojiunga A-level Sekondari ya Samora Machel, Mbeya wanatakiwa kwenda na matofali 300 - 500 ya fensi

KERO Wanafunzi wanaojiunga A-level Sekondari ya Samora Machel, Mbeya wanatakiwa kwenda na matofali 300 - 500 ya fensi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wanafunzi waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Samora Machel, Mbeya, wanatakiwa kuchangia matofali 300 kwa wale waliochaguliwa moja kwa moja na matofali 500 kwa wanafunzi wanaohamia kutoka shule nyingine, kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule.

Sasa, kama elimu ni bure, mzazi kama mimi ambaye kipato changu hakitoshi kukidhi mahitaji ya mtoto shuleni, nitapata wapi fedha za kununua matofali 300 kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule? Nimepanga vyumba viwili vya kuishi, sasa nitatoa wapi uwezo wa kugharamia ujenzi huo?

Jukumu la kujenga shule ni la nani? Kwa nini mzazi alazimike kutumia gharama za kununua na kusafirisha matofali hadi shuleni kwa ajili ya ujenzi? Matofali 300 yanaweza kugharimu takribani Sh300,000, bila kujumuisha mahitaji mengine ya mwanafunzi kama madaftari na sare za shule. Mimi, kama mzazi, nimetumia miezi kadhaa kuweka akiba ili mtoto wangu apate sare za shule. Sasa nitapata wapi fedha za kugharamia ujenzi wa ukuta wa shule?

Ni wakati sasa kwa Serikali kuangalia upya vipaumbele vyake. Kama kipaumbele ni kuwastarehesha watawala na wafanyakazi wa Serikali, basi hilo lielezwe wazi. Lakini kama lengo ni kuwahudumia wananchi, Serikali inapaswa kutekeleza wajibu wake ipasavyo, badala ya kuendelea na mfumo unaowaongezea wananchi mzigo wa gharama huku wakihangaika kukidhi mahitaji yao ya msingi.
 
Tsh 300,000 tu mtu anakuja kupiga umbeya namna hii.

Shule anayosoma mtoto wa Dejembi au Heche sio tu ina ukuta ina mpaka CCTV cameras kutazama usalama wa watoto wao. Na wanalipa sababu wanajua elimu ni gharama.

Wewe endelea kuonesha ujinga wako ukifikiri unaleta malalamiko ya maana.
 
Ahaaaa ahaa ila wazazi wa siku hizi mchango kidogo malalamiko ya kutosha.

Ukuta si utawasaidia watoto wao ulinzi na utulivu ili wasome vizuri?
 
Tsh 300,000 tu mtu anakuja kupiga umbeya namna hii.

Shule anayosoma mtoto wa Dejembi au Heche sio tu ina ukuta ina mpaka CCTV cameras kutazama usalama wa watoto wao. Na wanalipa sababu wanajua elimu ni gharama.

Wewe endelea kuonesha ujinga wako ukifikiri unaleta malalamiko ya maana.
Wewe ukiona unaimudu jua kuna wenzako hawawezi kuimudu so tulia
 
Serikali inatakiwa kutimiza majukumu yake...otherwise irudishe ada ili ada ifanye majukumu hayo!
 
Back
Top Bottom