Kyambamasimbi
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 762
- 1,597
Habari wanaJF.
Jamani, nimeexperience mara kadhaa nikiwa nasafiri barabara ya Iringa kutoka Morogoro, huwa naona watoto wadogo wa shule ya msingi Msimba wakitembea umbali mrefu kufuata shule iliko. Mbaya zaidi, wakati wa masika huwa wanatia huruma sana watoto hawa, na huwa wananyooka wakitembea pembezoni mwa barabara kuu yenye malori na mabasi.
Jamani, mwenzenu huwa naumia moyo juu ya watoto wale. Kuna siku nilimuomba dereva awabebe, na nilivyowashusha walifurahi na kushukuru kwa kupiga magoti. Jamani, kimoyomoyo niliwaombea, "Eeeeeee Mungu, wakumbatie watoto wako."
Serikali, wasogezee watoto hawa shule angalau wafarijike wajione ni sehemu ya Watanzania. Jamani, huwa naumia sana sijui kwa sababu nimekulia shida?
Naomba kuwasilisha.