Hao Wanafunzi nami nimewahi kuwaona mara kadhaa wakiomba hata lift kwenye mabasi ama magari binafsi ili waelekee Shule.
Sisi tuliokua zamani, ilikuwa tunasafiri Umbali kama huo ama zaidi ili kwenda Shule, lakini haifai maisha yale na Vijana wetu wayaishi.
Halmashauri inakusanya mapato, lakini pia hata Serikali KUU ione namna ya kusaidia kumaliza hili tatizo.
Shule inaitwa Msimba Shule ya Msingi, Ipo kwenye Kata ya Mikumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa. Ni Moja wapi ya Shule za zamani zamani kidogo, nahisi kwenye miaka ya 2000 hivi imeanza
DED, Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Mbunge wa Jimbo la Mikumi waone namna ya kusaidia kuondoa hili tatizo.
bitimkongwe Lucas Mwashambwa