Wanafunzi wanaotia mimba walimu nao waendelee na masomo?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Kumekuwa na mkanganyiko kuhusu mimba mashuleni ambapo tafsiri na mitazamo huelemea wanafunzi wa kike wanaopewa mimba na watu (wakiwemo Walimu) huku wanafunzi wa kiume wanaotia mimba Walimu wao wa kike wakiachwa nje ya tafsiri na mitazamo hiyo.

Zipo jamii katika nchi za Tanzania na Kenya ambapo kwa mujibu wa mila zao e.g. Wakurya, unakuta mwanafunzi wa kiume ameoa Mwalimu wake na anaendelea na masomo kama kawaida.

Aidha, nimewahi kushuhudia kesi ambapo wazazi wanapinga kufukuzwa shule mtoto wao wa kiume kwa kosa la kumtia Mwalimu wake mimba; wakidai kwamba Mwalimu ndiye afukuzwe kazi badala ya mwanafunzi kwamba utovu wa nidhamu hauko kwa mwanafunzi bali kwa Mwalimu wake huyo.

Waraka wa Waziri wa Elimu (hivi karibuni) kuhusu wanafunzi wenye mimba kuendelea na masomo haukujibu maswali ya tafsiri na mitazamo hiyo.



Taswira kwa hisani ya google
 
Ndio masomo ya kujua namna ya kumtunza mwalimu wake kwenye ndoa.
 
Na je, wanafunzi/watoto wadogo walioko jela za watoto nao waendelee na masomo wanapotumikia vifungo vyao?
 
Tafsiri sahihi ni kwamba huyo mwalimu mtiwa mimba kambaka mwanae. Mwalimu ametumia nafasi yake kumlazimisha mtoto amkoyonge !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…