Wanafunzi Wavamia Tume ya Vyuo Vikuu - TCU

Wanafunzi Wavamia Tume ya Vyuo Vikuu - TCU

SuperNgekewa

Member
Joined
May 10, 2010
Posts
49
Reaction score
3
WANAFUNZI WAVAMIA TUME YA VYUO VIKUU


WANAFUNZI WAVAMIA TUME YA VYUO VIKUU - TCU - 1.JPG
Baadhi wa wanafunzi wakiwa nje ya jengo hilo.

KUNDI la wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kujiunga na vyuo mbalimbali vya serikali na kupata alama za juu leo wamefurika nje ya Jengo la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) lililopo Mikocheni jijini Dar es Salaam wakipinga uamuzi wa wenzao waliopata alama ndogo kupatiwa nafasi za kujiunga na vyuo vya serikali na wao kukosa nafasi na kudai uamuzi huo ni wa kuwaonea.


WANAFUNZI WAVAMIA TUME YA VYUO VIKUU - TCU - 2.JPG
Askari wa jengo hilo akiinyoosha mkono kuwataka wanafunzi hao kukaa mbali na eneo hilo, amri waliyokataa kuitii.​


WANAFUNZI WAVAMIA TUME YA VYUO VIKUU - TCU - 3.JPG

Muuza "lamba-lamba" (ice cream) akiwa kwenye mkusanyiko huo kukata kiu ya ‘madenti' hao.​



PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY
 
TCU sio Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Bali ni Ka tume ka VYOO VIKUU TANZANIA. Hawana Hadhi ya kusimamia VYUO Vyetu.:mad2:
 
Ndio muelewe jinsi jamaa wanavyochakachua hata usaili.Huu ndio mfumo tuliouchagua sisi wenyewe msilalamike.Wakati jamaa walipokupa 5,000/= na tshirt ulifikiri nini.Hao ni wazee wetu waliposhindwa kujua na njaa yao wakauza haki yao.Wanafunzi msiondoke mpaka kieleweke
 
Back
Top Bottom