Habari ya mtoto kufundishwa kufanya kazi toka mdogo mie naiona sehemu ya grooming and upbringing! Usiniambie kama mtoto kufagia, kuchota maji na kidumu kama ikihitajika ama kulima kiasi ni child labor! Hivi vitu vinamfundisha mtoto discipline na kumuandaa kujitegemea baadae. Mfano, baada ya kuhusika kikamilifu na ufuaji wa nguo zangu za shule I was extra careful kuhusu kuchafua manake najua mziki wake!
Muhimu mtoto apewe elimu ya ukimwi na situation aliyo nayo! Afundishwe kujilinda na maambukizi mapya na kuwalinda wenzie both nyumbani na shuleni. Sioni any connection btn kufagia na hiv, inakuwa kama mnamuandaa kufa tu na hahitaji life skills! Shame Kiranga!
Naelewa yote hayo, ndiyo maana ukifuatilia thread utaona namulika dichotomy ya kukubali tunayoletewa na western world au kuamua wenyewe?
Ndiyo maana hiyo "child labor" nime i qualify kwamba "kuna wengine watasema" kwa kujua kwamba katika context ya kitanzania mtoto kufundishwa kazi ni wajibu kama ulivyosema hapo juu.
Katika context ya kiTanzania, ugonjwa si kitu cha kuonewa aibu (UKIMWI/HIV ni ugonjwa mpya na kama alivyosema Mwinyi "umekaa pabaya" kwa hiyo una anomalous stigma), na privacy hatuijuhi kama wanavyoijua hao watu wa West.
Kwa hiyo kuna a separate line of thinking inayokuja hapa, kwamba, jamii ya Kitanzania inawezekana in a dilapidated way, in it's own context,imeendelea sana kupita hao watu wa magharibi kiasi cha ku prioritize kitu muhimu kabisa, afya na maisha ya mtoto, kuliko kitu ambacho katika jamii ya kitanzania hakina umuhimu mkubwa, privacy.
Inawezekana hawa watoto wanajulikana tayari kwamba ni HIV positive kijiji kizima kwa sababu kila mtu anajua walizaliwa wakati wazazi wao wana HIV. Kwa mtoto kama huyu, kitu muhimu ni nini, privacy au protection?
Ni swali gumu kwa sababu jamii zetu ziko nyuma kiuchumi kiasi kwamba tunaona hata tamaduni zetu ziko nyuma, na inawezekana nyingine zipo nyuma.
Lakini je, hili linamaanisha Waswede Wamarekani na Waingereza ambao tamaduni zao zina expectations zaprivacy level iliyo unrealistic kwetu wana haki ya kututaka tuwe na privacy kama yao?
Wwana haki ya kusema privacy expectations za tamaduni zao ndio ziwe standards za dunia?
Wengine wanaweza kusema tukitaka kufuatisha sana standards za west tutafikia point mtu ana mgonjwa mahututi, ambulance limekuja kumchukua kumpeleka hospitali, tunakataa kumpandisha mgonjwa mahututi kwenye ambulance kwa sababu halina reflective sticker au halijafanyiwa inspection katika miezi 6 iliyopita kama kinavyosema kitabu cha code za ambulance maintenance cha California, huku sie tuko Malampaka.
Hii epidemic inaweza ku warrant exceptions kwa watu wanaoamua kusema mie privacy kwangu si muhimu kama kupata nafasi ya kutofagia na kuchokoza magonjwa zaidi?
Hii aproach ya kibongobongo, hata kama ni serendipitously, inaweza kuondoa stigma juu ya UKIMWI/HIV kwa kuonyesha kwamba UKIMWI ni ugonjwa kama asthma tu? Na kama tunaweza kuwapa exception watoto wenye asthma, tunaweza kuwapa wenye UKIMWI pia (labda tuwavishe wagonjwa/ waathirika wote label, tuna solve tatizo la kuwanyanyapaa wenye UKIMWI tu)
Lakini hata ukiwawekea label wagonjwa wote, bado watu wenye values za kimagharibi watasema mnanyanyasa wagonjwa fundamentally, despite the practical reasons.
Hivi bongo kama jamii tuna value privacy kihivyo? Mtu mwingine ukimsalimia na kumjulia hali rhetorically tu ataanza kukuelezea mgongo unavyomuuma na kukupa his entire medical history, mtu kama huyu ukimwambia unarisk mtoto apate magonjwa kwa sababu ya privacy atakuelewa?