Wanagawiana hadi ndege Tausi, hawawezi kutusikia hao!

Wanagawiana hadi ndege Tausi, hawawezi kutusikia hao!

Watu wa Pwani mara nyingi wakiongea huwa wanaongea kwa mafumbo na inabidi uwe mchokochoko kidogo ili uelewe nini kinaongelewa, sasa mie toka ile shughuli ilivyoisha mie najiuliza maana ya " Nimejifunza ndege hawa usiku hupenda kulala juu ya miti na kuacha vifaranga chini na asubuhi hushuka chini akivikuta vifaranga vyote haya vikipungua haya" hii ni kwa nukuu yangu toka Chalinze Chalinze hivi
Mafumbo yanawasidia nini
 
Pale Ikulu enzi ya Mwalimu hapakuwa na ndege aina ya Tausi tu bali kulikuwa na MINI ZOO ya wanyama . Kulikuwepo Kongoni , digidigi na wanyama wengine wa porini , sasa najiuliza wale wanyama walipotelea wapi na lini? Ikulu hakukuwa na TAUSI peke yake!!!
 
Mambo mengine tuwe tunaacha yapite mkuu. Tausi si kitu kikuuuuubwa
Ni kitu kidogo lakini kitendo walichofanya kinaonyesha uhasilia ya viongozi wetu wanaojiita viongozi wa wanyonge. Unajua mtu naweza jambo dogo sana lakini likaonyesha ni mtu wa namna gani.
 
Walivyoelezea tu historia ya ujio wa makao Makuu Dodoma na hasa kila mmoja alivyogusia alichokifanya utagundua kabisa wapo pamoja. Kubwa zaidi ni namna walivyozawadiwa zawadi ya ndege. Utasema nini sasa?

Mkulu akaona afanye justification asionekane kajipendelea yeye tu kuhamishia wanyawa kule kwake. Kawapa na wenzake na hamna aliyekataa though Mkwere kdg alionesha wanaweza kwenda kufa kwake.

Sasa hapa najiuliza iwapo hawa watu wapo wamoja hivyo kwa mambo yasiyo na manufaa kwa wananchi yaani hadi kupeana tausi - ndege wa kifahari namna hivyo wanaashiria nini sasa ukifanya na ulinganisho wa kubinya haki za wafanyakazi. Mfanyakazi hajapandishiwa mshahara miaka minne - hivi Mkwere kwa nini pale hata hukusema hilo?

Mkapa kwanini usingeshukuru kwa zawadi ya tausi halafu ukamchomeka basi mwanao awakumbuke hata wafanyakazi tu? Mzee Mwinyi umezibwa mdomo sio!

Sasa hao tausi wanasaidia nini sasa kwako kuishi kwa amani na raha mustarehe kama kuna wastaafu wenzio hawajalipwa tangu wastaafu mwaka jana Julai?

Mnawapamba wanajeshi kuwa wanafanya kazi nzuri ili kuwajaza mioyo ya kuwachukia wale wanaowakosoa! Mnawaahidi kazi JKT na mnawapandisha vyeo lukuki.

Wafanyakazi wengine mnawanyima nyongeza, mnawahamisha bila kuwapa haki zao, mnawakaimisha hadi matako yanaota sugu bila kuwathibitisha, hamtoi ajira mpya, yaani ni full manyanyaso!

Anyway endeleeni tu kula nchi na ndege wake - ipo siku mambo yatabadilika tu- oneni ya USA. Ukweli na mwaka huu chama changu CCM sikipi kura hata moja, hata kama kijijini kwangu Idukilo kitawapata wanaCCM loyal kwenu. Mimi hapana!
Ingekuwa kwenye nchi kama Namibia au Botswana ambako democracy iko juu hiki kitu hakiwezi tokea. Sana sana kama wako wengi na Ikulu imezidiwa wangefanya mnada ili mwenye pesa zake awanunue. Tausi ni mali ya umma siyo ya mtu binasfi kama jamaa yetu anavyofikiria.

Mwalimu angkuwa hai sidhani kama angekubaliana na hicho kitu ......!!
 
Ingekuwa kwenye nchi kama Namibia au Botswana ambako democracy iko juu hiki kitu hakiwezi tokea. Sana sana kama wako wengi na Ikulu imezidiwa wangefanya mnada ili mwenye pesa zake awanunue. Tausi ni mali ya umma siyo ya mtu binasfi kama jamaa yetu anavyofikiria.
Nilimsikia mshikaji chizi mmoja wa NCCR Mageuzi akisema eti NCCR wakiongoza nchi lazima Ndege Tausi warudishwe. Hata kama ni kwa kuwatapika!
 
Pale kwenye sherehe Nilimsikia mtu mmoja akimnong'oneza mwenzake kwamba thamani ya tausi mmoja ni kubwa kuliko watanzania wanyonge wawili
 
Pale kwenye sherehe Nilimsikia mtu mmoja akimnong'oneza mwenzake kwamba thamani ya tausi mmoja ni kubwa kuliko watanzania wanyonge wawili
Issue wala sio thamani lkn ni kitendo chenyewe kinaashiria nini kwenye Jamii zetu hizi. Mie kwangu naona kama vile Magu anawapaka matope tu wenzake - yaani aanafunika vitendo vyake vya hovyo vya kuhamisha wanyama toka mbuga hii kupeleka kule kwake. Sifikirii kama kile kitendo kimefanyika kwa roho nyeupe - wamekubali basi tu (hasa mjanja JK) lakini basi imeshafanyika.
Rais aliteumikia nchi yake vizuri hutamani arudi maisha yake yale yale ya zamani yenye amani tele. Sasa hapa unapompelekea Tausi wa Ikulu unaashiria nini sasa?
 
mi JK angerudisha fadhila kwa kumpa jpm Kasuku!ili jpm ajifunze kuhutubia Kasuku wanafaa kwa kujifunzia lugha!!
 
Wewe ukipewa utawafugia wapi hata pa kulala huna

Mkuu hao hata ukiwatandikia kitanda ndani wao watatoka nje kwenda kulala kwenye miti nje kwani asili yao ni porini kama kanga na kufugwa ni bahati mbaya au mwenzetu hujawahi kuwaona wakilala kwenye miti ya pale Ocean Road Hospital?
 
Back
Top Bottom