Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mmoja wa wadau katika warsha ya uandaaji wa maudhui ya ndani iliyoandaliwa na TCRA alionesha masikito yake kuwa analazimika kuandaa vipindi vinavyotetea tozo japo yeye binafsi hakubaliani na tozo za kwenye miamala ya fedha kwenye simu na benki.
Mdau huyo amesema " Nazungumza uongo mbele ya 'Audience' yangu, nafanya kipindi kuhusu tozo, tozo yenyewe mimi inaniumiza maana mimi mshahara wangu unakatwa na ukienda benki unakatwa tena halafu nalazimika kusema tozo ni nzuri" Alisema mdau huyo kwenye warsha.
Serikali ilianzisha kukusanya kiasi cha pesa kwenye miamala yoyote ya kutuma na kutoa fedha kwa njia simu na benki ambayo imeibua mjadala mkubwa kwa wananchi ambao hawajaridhishwa na uwepo wa tozo huku wengi wakitaka tozo hizo kuondolewa na Serikali.