SI KWELI PreGE2025 Wanahabari wasusia shughuli za CHADEMA kisa kauli ya Tundu Lissu

SI KWELI PreGE2025 Wanahabari wasusia shughuli za CHADEMA kisa kauli ya Tundu Lissu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimekutana nayo kuwa Katika hatua isiyo ya kawaida, wahariri na waandishi wa habari wamesusia shughuli zote za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kauli tata ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

WANAHABARI_CHADEMA_27MAR25.jpg
 
Tunachokijua
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ni asasi isiyo ya faida iliyoanzishwa na wanachama wa hiari kutoka miongoni mwa wahariri, viongozi wa vyombo vya habari, waandishi wa habari wakongwe, na wakufunzi wa uandishi wa habari kutoka sekta ya vyombo vya habari nchini Tanzania.

Madai
Ipo taarifa inayodai kuwa wahariri na waandishi wa habari wasusia shughuli za CHADEMA, taarifa hiyo inaambatana na barua inayodaiwa kuwa imetolewa na Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF). Tazama hapa na hapa

Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa haina ukweli. Ufuatiliaji umebaini kuwa barua hiyo haijatolewa na Jukwaa la wahariri hivyo ni ya kughushi.

Madai ya Lissu kuwaambia waandishi wa habari hawana akili na ni maadui wakubwa wa maendeleo ya wananchi si ya kweli. Lissu alipokuwa katika mkutano huo Sumbawanga alizungumzia vitu tofauti ikiwemo ajenda yao ya No reforms na No election na hakuzungumzia jambo lolote kuhusu waandishi wa habari kutokuwa na akili. Tazama mkutano huo hapa.

JamiiCheck pia imefautilia grafiki ambayo inaonekana kuw ana nembo ya Millard ayo na kubaini kuwa haijachapishwa na Millard Ayo. Grafiki hiyo pia ina makosa baadhi ikiwemo ya kiuandishi mfano neno “kutoka” imendikwa neno “kuroka”

Aidha Jukwaa la wahariri limekanusha kuhusu Taarifa hiyo na barua hiyo.
Back
Top Bottom