Hali ya wasiwasi imeongezeka Homa Bay huku maandalizi ya ziara ya Linda Mwananchi yakizua mvutano katika mji huo.
Wanahabari wawili wa AFP, Fred Ooko na Brian Ongoro, walishambuliwa na kundi la vijana waliokuwa na silaha walipokuwa wakiripoti hali ya usalama katika mji wa Homa Bay. Kwa mujibu wa taarifa, walipigwa kwa marungu na kuvutwa barabarani kabla ya kuokolewa na mwendesha bodaboda.
Washambuliaji pia wanadaiwa kuchukua vitambulisho vya waandishi wa habari, leseni za udereva, kamera pamoja na mali zao nyingine. Wanahabari hao baadaye waliripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi cha Homa Bay.
Wakati huo huo, shughuli za kawaida katika mji huo ziliathirika. Baadhi ya vijana walifunga barabara, huku usafiri wa umma na biashara zikisimama katika maeneo kadhaa. Baadhi ya makanisa pia yalifungwa kutokana na hofu za kiusalama.
Tukio hilo linatokea wakati viongozi wa Linda Mwananchi, akiwemo Edwin Sifuna, James Orengo, Babu Owino, Caroli Omondi na George Natembeya, wakiendelea na ziara yao katika eneo la Suba South, ambapo mikutano ya hadhara ilipangwa kufanyika Nyandiwa na Sindo.