Wanaharakati, mbona hamsemi kinachoendelea kwa “Mwalimu” wenu Hakainde Hichilema?

Wanaharakati, mbona hamsemi kinachoendelea kwa “Mwalimu” wenu Hakainde Hichilema?

Irene Darton

Member
Joined
Feb 25, 2024
Posts
27
Reaction score
32
Na: Chris Bwaya Chilumba
31.08 2026

Mwaka 2017, HH akiwa mpinzani nchini Zambia, alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini.

Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa kuhusu matumizi ya sheria dhidi ya wapinzani na hatimaye mashtaka yakaondolewa.

Mwaka 2021, baada ya Hichilema kushinda urais, baadhi ya wapinzani na wanaharakati Tanzania walimshangilia sana.

Maria Sarungi Tsehai kwa mfano, aliandika: “Safi sana HH, show them how it’s done!”

HH akaonekana kama mfano wa mwanasiasa aliyepambana na dola na hatimaye akaingia Ikulu. Lakini leo, akiwa Rais, Brian Mundubile, mpinzani wake, amefunguliwa mashtaka ya uhaini.

Hapo ndipo tunapaswa kujiuliza: je, Principle bado ni principle wakati “mtu wetu” anapokuwa upande wa dola?

Tusichanganye mambo: Uhaini si kosa maalum kwa wapinzani, wala upinzani si kinga dhidi ya jinai.

Mtu yeyote anayefanya kitendo kinachokidhi vigezo vya kisheria anapaswa kuchunguzwa na kama ushahidi upo, kushtakiwabila kujali cheo chake.

Lakini pia mashtaka si hukumu. Mundubile anapaswa kupatiwa 'due process', Serikali iweke ushahidi wake mezani na mahakama iamue.

Hii ndiyo maana ya rule of law: si “mtu wangu akifanya ni haki, mtu wao akifanya ni jinai.”

Mwanaharakati wa kweli hatakiwi kumtetea mtu kwa sababu tu ni mpinzani; anatakiwa kutetea haki yake kwa sababu ni haki. Leo unaweza kumtetea mpinzani kwa sababu ni mpinzani, kesho akawa Rais na akamfungulia mpinzani mwingine mashtaka yale yale uliyokuwa ukilalamikia.
Hapo ndipo unagundua kama ulikuwa unatetea principle au ulikuwa unatetea upande.

Tuwatazame akina John Heche, Maria Sarungi, Hilda Newton, Tito Magoti, Twaha Mwaipaya na wengine waliowahi kuitazama Zambia ya HH kama mfano wa kisiasa. 😃

Tunawauliza, Mnaionaje Zambia ya leo? 😃

Mnamuonaje HH, yule ambaye mwaka 2017 alijikuta akikabiliwa na uhaini akiwa mpinzani, leo akiwa Rais na mpinzani wake akikabiliwa na mashtaka hayo hayo? 😃

Je, kama Serikali ina ushahidi, mnaunga mkono mchakato wa sheria? 😃

Kama mnaona kuna matumizi ya dola kisiasa, mbona hamsemi kwa nguvu ile ile? 😃

Na kama bado mnachunguza, semeni. 😃

Msitutazame tu kama mlivyokuwa mkituambia “Look at Hichilema.” 😃

Tumemuangalia. Sasa tunawaangalia nyinyi. 👀

Kwa sababu hili si suala la kumpenda au kumchukia HH, wala kumpenda au kumchukia Mundu.

Wanaharakati mna mtihani wa consistency.

Wanaharakati msiwe mashabiki wa wapinzani; kuweni mashabiki wa haki.

Wanaharakati wasimtete mtu kwa sababu ana cheo cha mpinzani, bali kwa sababu hoja yake inastahili kutetewa na wasiishambulie Serikali kwa sababu tu ni Serikali, bali pale inapokiuka principle wanazodai kuamini.

HH wa 2017 alistahili haki. Mundu wa 2026 pia anastahili haki.

Na kama kuna ushahidi wa uhaini, sheria ichukue mkondo wake.

Sasa swali ni moja tu: Je, principle zenu ni principle kweli au zinabadilika kulingana na nani anakidhi maslahi yenu ya kufanya harakati? 😃😃
 
Na: Chris Bwaya Chilumba
31.08 2026

Mwaka 2017weli au zinabadilika kulingana na nani anakidhi maslahi yenu ya kufanya harakati? 😃😃
Hata Lissu akija kuwa rais halafu abadilike hatutaendelea kumchekea tutamgeuka tu. Atasifiwa kwa mazuri akiboronga hatutaendelea kumtetea tutamuondoa na kumuweka mwengine.

Upo hapo wee kayngay?
 
Hata Lissu akija kuwa rais halafu abadilike hatutaendelea kumchekea tutamgeuka tu. Atasifiwa kwa mazuri akiboronga hatutaendelea kumtetea tutamuondoa na kumuweka mwengine.

Upo hapo wee kayngay?

Wewe unasema hivyo…. Lakini sio kwa viongozi wa chadema wenye maslahi binafsi
 
Wewe unasema hivyo…. Lakini sio kwa viongozi wa chadema wenye maslahi binafsi
Kwahiyo, wewe unapendekeza nini sasa?, wenye maslahi CCM pekee ndio waendelee kututeka na kujilimbikizia malli sio!!! Huna solution zaidi ya kudandia tu kama ma-three (Matatu).
 
Kwahiyo, wewe unapendekeza nini sasa?, wenye maslahi CCM pekee ndio waendelee kututeka na kujilimbikizia malli sio!!! Huna solution zaidi ya kudandia tu kama ma-three (Matatu).
Solution katika Africa ni Mgombea huru tu.
 
Solution katika Africa ni Mgombea huru tu.
"Power without control is chaos", ushawahi imagine mtu yupo Top na hana wa kumuambia shit? ndio hayo ya CCM sasa tunayoyaona ya rais kuwa mwenyekiti wa chama, haina utofauti na kuwa mgombea huru, maana mwenyekiti yupo huru kufanya atakalo, ukizingua anakuvua uanachama. Hata USA wana mgombea huru, ila ni rais wa kwanza pekee George Washington ndio aliongoza nchi kama mgombea huru. hawajawahi mpitisha tena mtu kuwa raisi akiwa huru, hata aliyekuwa maarufu sana Ross Perot hakushinda jimbo hata moja.
 
Mfano wa Samia ni kielelezo cha kutoruhusiwa mgombea huru. Kila mtu ambaye anapigania tumbo lake, anaogopa kumwaga ugali kwa kumweleza kiongozi ukweli (maana wakichukua kadi yao, na uongozi bye bye-mfano Dr Nchimbi). Akiwa anaruhusiwa, basi Samia hata awe Mweyekiti, akimfukuza anahamia chama kingine! Uhuni wa hivi sasa TZ ungeisha.
 
Back
Top Bottom