Wanaharakati Myanmar waitisha kampeni mpya dhidi ya Jeshi

Wanaharakati Myanmar waitisha kampeni mpya dhidi ya Jeshi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Myanmar Nach dem Militärputsch

Wanaharakati wanaopinga utawala wa kijeshi nchini Myanmar wamewataka watu kuacha kulipa bili za umeme na mikopo ya kilimo, na kutowapeleka watoto shuleni, wakipinga ahadi ya kiongozi wa kijeshi ya kukomesha mzozo.

Maandamano ya hapa na pale yalifayika katika miji mikubwa nchini Myanmar jana Jumapili, siku moja baada ya Jenerali mwandamizi Min Aung Hlaing kufikia makubaliano ya kukomesha mzozo, wakati wa mkutano wa kilele wa viongozi wakuu wa mataifa ya jumuiya ya ushirikiano wa kusini mashariki mwa Asia, ASEAN, uliofanyika nchini Indonesia wiki iliyopita.

Utawala huo wa kijeshi haukusalimu kwa miito ya kuwaachia wafungwa wa kisiasa, akiwemo kiongozi wa serikali ya kiraia Aung San Suu Kyi, na makubaliano hayo ya ASEAN yalikosa ratiba yoyote ya kukomesha mzozo.

Siku ya Jumatatu utawala huo wa kijeshi uliahirisha tena kesi ya mahakamani dhidi ya Aung San Suu Kyi, wakati mawakili wakipambana kupata ruhusa ya kumtembelea, wiki 12 tangu alipokamatwa.

Indonesien Tangerang ASEAN-Gipfel | General Min Aung Hlaing Myanmar
''Kesi iliahirishwa hadi Mei 10 kwa sababu ya suala moja tu: kuhusu jibu la polisi juu ya iwapo kuwekwe utaratibu wa mkutano kati ya washtakiwa na mawakili,'' alisema mmoja wa mawakili hao Khin Maung Zaw.

Mawakili hao waliomba mkutano kama huo mapema, lakini mahakama ilikuwa haijawakubalia ombi lao.

Urusi yasema inapendelea suluhisho la ndani​

Suu Kyi anakabiliwa na jumla ya mshtaka sita, yakiwemo ukiukaji wa sheria za biashara ya nje, kuhusiana na vifaa vya mawasiliano ya redio za mkononi vilivyokutikana nyumbani kwake na kukiuka vikwazo vya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Mashtaka mazito zaidi mpaka sasa ni kuhusu uchochezi wa uasi.

Kundi la wanaharakati wa ufautialiaji linasema watu 751 wameuawa na vikosi vya usalama katika matumizi ya nguvu ya majenerali dhidi ya maandamano endelevu yalioanza tangu mapinduzi ya Februari Mosi.

Myanmar Protest in London

Waandamanaji wakibeba mabango ya kuomba msaada kwa jumuiya ya kimataifa kuinusuru Myanmar kutokana na utawala wa kijeshi.​

Kampeni ya uasi wa umma imezorotesha uchumi, na mashirika ya kimataifa ya misaada yameonya juu ya uwezekano wa kuzuka njaa.
Wanaharakati wa demokrasia wametoa wito wa kuimarisha juhudi zao siku ya Jumatatu, kwa kukataa kulipa bili za umeme na mikopo ya kilimo, na kwa watoto kuacha kwenda shuleni.

Ikulu ya Urusi, Kremlin, imesema leo kuwa inapendelea suluhisho la ndani kwa mzozo wa Myanmar, huku ikisema pia kwamba Urusi inalaani vikali vitendo vyovyote vinavyosababisha vifo vya raia.

Mapema mwezi huu, Urusi ilionya kwamba vikwazo dhidi ya watawala wa kijeshi nchini Myanmar vinaweza kuisukuma nchi hiyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Kwanini wasiitishe tu uchaguzi ama wamwache mama amalizie kipindi chake ..Sijui jeshi linataka hii nchi iingie kwenye vita.
 
Hawa wajeda wananiangusha sasa

Wangechinja tu hao wauaji waliiwaeka ndani shughulu iishe.

Wanawabembeleza bure tu hao waliua wengi sana na hao wanaharakati walikua kimyaaaaa eti leo wanatetea wauaji wenzao
Pambaf kabisa maliza wote na kila anaeunga mkono wanajiona wao ndio wana haki ya kuishi tu na wengine ni takataka

Big up jeshi
 
Back
Top Bottom